Mgomo wa Wafanya Biashara Mwanza

Mgomo wa Wafanya Biashara Mwanza

Ndengaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2014
Posts
7,831
Reaction score
14,259
Kuna Mgomo wa Wafanya Biashara unaendelea Mwanza sasa hivi, Mliopo Mwanza toeni update nini kinaendelea.

Video nimeweka hapa Chini.



************************************************************************************************************
Update Kutoka Mwananchi Digital

Siku moja baada ya wafanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es Salaam kugoma na kufunga maduka, wafanyabiashara jijini Mwanza nao wamefunga maduka.

Mwananchi Digital imepita katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo na kubaini kutofunguliwa kwa maduka katika baadhi ya mitaa ikiwamo ya Kaluta, Rwagasore, Nyerere Plaza, Uhuru, Liberty na Kenyatta.

Chanzo Chatajwa

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Mwanza, Patrick Masagati ametaja sababu za mgomo huo.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumanne Juni 25, 2024, Masagati ametaja sababu hizo kuwa ni kupinga sheria za kodi (bila kuzitaja) zinazochangia unyonyaji na kuwarudisha nyuma wafanyabiashara.

"Kitu ambacho kimewasukuma wafanyabiashara kusitisha biashara zao ni yale yanayoendelea kuhusiana na sheria za kodi. Sheria za kodi zimekuwa tatizo," amesema Masagati.

Alipoulizwa ukomo wa mgomo huo, Masagati amesema hawezi kuweka wazi lini utakoma kwa kile alichodai jukumu la kusitisha mgomo huo limekabidhiwa mikononi mwa wafanyabiashara wenyewe.

"Baada ya kuwasilisha kero na changamoto zinazowakabili wafanyabiashara kwenye mamlaka za Serikali na kurejesha tuliyoyapata serikalini, kwa hiyo wameona hatua zaidi ya kuchukua ni kusitisha biashara zao,” amesema Masagati.

Baadhi ya maduka yakiwa yamefungwa jijini Mwanza. Picha na Mgongo Kaitira

“Malalamiko na matamanio ya wafanyabishara ni kuona sheria zinazosimamia wafanyabiashara zinarekebishwa. Na kwa sababu leo Waziri wa Fedha anawasilisha bajeti ya Taifa, tunaamini kwamba yale ambayo wafanyabiashara wanayalalamikia yatarekebishwa,” amesema Masagati.

Uamuzi wa wafanyabiashara kufunga maduka yao umeacha maumivu kwa wafanyabishara wadogo ‘Machinga’ na wachuuzi wa bidhaa kutoka mikoa ya jirani na Mwanza ambao wamesafiri umbali mrefu kununua bidhaa jijini humo na kukutana na ‘makufuli’ katika milango ya maduka.

Machinga kutoka wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza, Enock Timba amesema mgomo huo umemsababishia athari kwa kile alichodai pamoja na kufika katikati ya jiji saa 12:30 asubuhi kwa lengo la kununua bidhaa, ameishia kuzunguka tu bila kuona duka lililofunguliwa.

“Sikutegemea kama nitakutana na mgomo nimeathirika sana, inabidi nizunguke sijui maduka yamefunguliwa wapi hata hivyo ninakoelekea sasa ni kurudi nyumbani sioni dalili za maduka kufunguliwa,” amesema Timba.

Mkazi wa Nyasaka jijini humo, Maria Nzemba amesema hofu yake ni namna gani atarejesha mkopo aliochukua kwa ajili ya kuanzisha biashara yake kwa kile alichodai amekosa bidhaa za kuzungusha katika eneo lake.

“Kwa kweli siku ya leo imetuathiri sana wafanyabishara wadogo, tuna mikopo, tuna watoto wanasoma na shule zinaenda kufunguliwa, maduka makubwa ambayo tunayategemea kununua bidhaa ili tuanze kuzungusha mitaani yamefugwwa tunaomba Serikali ifuatilie suala hili,” amesema Maria.

Mussa Fundikila kutoka Wilaya ya Chato mkoani Geita ameeleza kushangazwa na uamuzi huo wa wafanyabiashara huku akiumizwa kusafiri umbali mrefu hadi Mwanza na kukutana na mgomo huo.

Hadi kufikia saa 5:50 asubuhi, Mwananchi imeshuhudia hakuna dalili za wafanyabiashara kufungua maduka huku jitihada za kutafuta kauli ya Serikali kuhusiana na mgomo huo zikiendelea.
 
Wafanyabiashara Jijini Mwanza wameyafunga maduka yao kwa kile wanachoilalamikia masuala mbalimbali yakiwemo ya kikodi.



Siku moja baada ya wafanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es Salaam kugoma na kufunga maduka, hatimaye wafanyabiashara jijini Mwanza nao wamefunga maduka.
 
Kuna Mgomo wa Wafanya Biashara unaendelea Mwanza sasa hivi, Mliopo Mwanza toeni update nini kinaendelea.
Hizi ukifuatilia kuna chembe chembe za hujuma maana ukisikiliza hoja za wanaogoma ni mambo ambayo yanazungumzika mezani
 
Wafanyabiashara Jijini Mwanza wameyafunga maduka yao kwa kile wanachoilalamikia masuala mbalimbali yakiwemo ya kikodi.


Chanzo: ITV
Ngoja tuone mtawala na mtawaliwa nani mbabe.mwl aliyaona haya kitambo sana ndoa hakutaka wafanyabiashara/matajiri kuingia kwenye siasa.sasa ndo watajua nani aliyewaambia muwapenyeze matajiri kwenye siasa
 
Wafanyabiashara wengi sasa hivi wana stress kutokana na mauzo kuwa duni.
Unakuta mwezi umekatika hata mauzo ya 1M hayajafika japo bidhaa zako zimejaa dukani. Ila wakija TRA na Manispaa/Halmashauri wanataka chao.
Pia kodi ya service levy iliyowekwa na Halmashauri kwa kila mfanyabiashara kutoa ni total kodi kandamizi. Maana maelezo ya Kodi husika ukiyaangalia mfano usafi na ulinzi ni vitu ambavyo bado vinachangishwa nje ya hiyo kodi.
Serikali ikae na wadau kutatua changamoto ya mlundikano wa kodi na tozo Kwa wafanyabiashara.
Ikiwezekana TRA wafungue biashara zao kama ilivyo kwenye kilimo kuna shamba darasa kusudi waweze kuona changamoto wanazopitia wafanyabiashara.
 
Back
Top Bottom