Mgomo wa wafanyabiashara nchini

Mgomo wa wafanyabiashara nchini

Joined
Apr 11, 2024
Posts
24
Reaction score
55
Ndugu Zangu Wafanyabiashara. Nafahamu Maumivu Yenu. Hakuna Anayefungua Biashara Ili Afunge. Hakuna Anayepambana Ili Afeli. Hakuna Anayejitahidi Kupiga Hatua Ili Arudi Nyuma. Hata Sasa Naamini Mmejitoa Sadaka Kuonesha Hisia Zenu Za Maumivu Na Siyo Kwamba Mmetosheka Na Utafutaji. Maumivu Yenu Nayaelewa.

Ni Imani Yangu Kubwa Kuwa Serikali Yetu Ya Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania, Itaboresha Sheria Ya Ukusanyaji wa Kodi Na Kuweka Mazingira Rafiki Ya Biashara Zenu Ili Kusaidia Muweze Kuhimili Uendeshaji wa Biashara Zenu. Kwani Lengo La Serikali Ni Kuboresha Maisha Ya Wananchi Wake, Na Nchi Kwa Ujumla, Na Siyo Kuwadidimiza.

Ni Imani Yangu Kuwa Serikali Yetu Ya Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania, Ni Serikali Sikivu, Hivyo Itakuja na Njia Mbadala Wa Kutatua Changamoto Zenu, Ikiwa Pia Ninyi Ni Kitovu cha Ukuaji wa Pato La Taifa La Tanzania. Nikiwa Kama Kiongozi wa UVCCM Wilaya Ya Ilala, Lilipo Soko La Kimataifa, Kariakoo, Nafahamu UMUHIMU Wenu, Wafanyabiashara. TUNAWATEGEMEA SANA.

Ni Imani Yangu Kubwa Kuwa Hampuuzwi Hata Thumni Kama Mnavyoweza Kufikiria, Ndiyo Maana Kumekuwa Na Ujio wa Viongozi Kwenye Masoko Yenu, Mfano Mnamo Mwaka Jana (Mei, 2023), Kulikuwa Na Ujio wa Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Kusikiliza Changamoto Zenu. Hii Ni Ishara Ya Kwamba Mnathaminiwa, Na Kero Zenu Zinatafutiwa Mbadala, Ni Vile Si Kila Changamoto Huweza Kutatuliwa Kwa Wakati Mmoja, Hivyo Kulazimu Kuchukua Muda Kidogo.

Ni Imani Kubwa Kuwa Serikali Inaenda Kutatua Changamoto Zenu, Ikiwa Ni Pamoja Na Kufanya Mabadiliko Ya Sheria Ya Kodi, Pamoja Na Kuboresha Mazingira Yenu Ya Biashara. TUNAWATHAMINI. 🙏

Please #StopTheStrike

Naomba Kuwasilisha ✍️
#KaziIendelee🇹🇿
 
we mzee unaandika nini ?
WM alikuja mwaka jana hadi leo hakuna mabadiliko unaleta maswala ya imani hapa?
 
Ni Imani Yangu Kubwa Kuwa Serikali Yetu Ya Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania, Itaboresha Sheria Ya Ukusanyaji wa Kodi Na Kuweka Mazingira Rafiki
Janeth

Hiyo imani yako ni kwa serikali ipi? Maana vimekaliwa vikao zaidi ya 10 na wameendelea kudanganya wafanyabiashara na hakuna walichotimiza!.

Imani ya serikali gani?
Hivyo Kulazimu Kuchukua Muda Kidogo.
Lini?
Kumekuwa Na Ujio wa Viongozi
Ni ujio wa kiongozi na sio viongozi. Chalamila ni mtu asiye na hekima na busara ya kuongea mbele ya raia ndio maana hata wewe umeona aibu kumuweka.
Ni Imani Yangu Kubwa Kuwa Hampuuzwi
una maanisha nini? Mpaka sasa hakuna kiongozi aliyefika kusikiliza changamoto, halafu unasema hatpuuzwi! Una maana gani?
 
Janeth

Hiyo imani yako ni kwa serikali ipi? Maana vimekaliwa vikao zaidi ya 10 na wameendelea kudanganya wafanyabiashara na hakuna walichotimiza!.

Imani ya serikali gani?

Lini?

Ni ujio wa kiongozi na sio viongozi. Chalamila ni mtu asiye na hekima na busara ya kuongea mbele ya raia ndio maana hata wewe umeona aibu kumuweka.

una maanisha nini? Mpaka sasa hakuna kiongozi aliyefika kusikiliza changamoto, halafu unasema hatpuuzwi! Una maana gani?
unamueleza mtu asiyejua hata ni nini kinaendelea.
 
Mwaka jana waligoma wakasiliza Majaliwa tukajua Majaliwa yangeleta Suluhu leo bora muwalete Suluhu wamsikie Suluhu ipatikane wasije wakapaliwa na Pombe kama ya kipindi kile.
Hivi kwanza Air Hostes Yupo maana Hajasikika mda? au yuko mawinguni mpka atue chini atayapata hayo ya Kariakoo.

Salaamaleko
 
Kodi za Tanzania ni kama kuteka maji kwenye tenga
Unakusanya kodi vizuri tu, mwisho wa siku ripot ya CAG inasema tenga linavuja. Bora kufunga koki tusubiri mkingaji aweke ndoo
 
Back
Top Bottom