Mimi binafsi mtanzania nimemvualia kofia, hasa hasa sisi "WADANGANYIKA", wenzetu kule Zanzibar naona kama wana misimamo fulani wakati fulani. Linalonihusu hapa ni woga uliojengeka ndani ya mioyo na akili za watu. Kwa kweli huyu aliyeturoga tukafikia hatua hii ya akili zetu kuwa dhaifu kiasi cha kusahau na hata kutetea haki zetu alituweza.
Just imagine imagine katika kipindi cha miaka 5 baada ya uchaguzi mwananchi anataabika, hakuna ahadi zinazotekelezwa, kodi zetu zinaliwa na wajanja, hata wale tuliwapa dhamana ya kutulindilia hazina yetu wanaigeuka na kuanza kuitafuna. Lakini unapokuja wakati wa uchaguzi mtu anasahau kila kitu anachanganyikiwa na kuadaika na pesa/zawadi ndogo ndogo. Nina wasi wasi kama kweli hizi akili zetu zina uzalendon dani yake.
Kuhusa mada ya Mgomo, mimi binafsi ziwavunji moyo wale wachache wenye ujasiri, lakini nikionapo hapa serikali hii ilivyokuwa ya kisanii, itatoa vitisho na hata ikiwezekana kuwakamata viongozi wa TUCTA kama siom kuwaita chemba na kuwapatia fungu litakalowatoa umasikini, ambapo aidha hatutashangaa kusikia viongozi wakiahirisha mgomo, au wafanyakazi wachache kugoma.
Vinginevyo washikaji mgomo mwema