Mgomo wa Wahadhiri na Wanafunzi UDOM 2011

UDOM sasa wamekua tutawafiria kuwapandisha hadhi kutoka choo kikuu kuwa chuo kikuu
 
Mwambie huyo!!ujifunze kuhusisha ubongo usiwe ukawa kama lile Vuvuzela la CCM ulilolitaja awali.Bip up!
 
hali bado ni tete kwani wanafunzi wanaosoma college ya education waendelea kusimamia madai yao huku ikifikia ni wiki 1 huku mgomo hou ukiendelea

Jamani WANAFUNZI vp tena? Nakumbuka hapo zamani mkachangishana vijisenti ili mgombea wetu wa urais wa JMT atwae form kiulaini na kwamba alikuwa ndiye mtu sahihi kwa utatuzi wa matatizo ya nchi ikiwemo hayo yanayosumbua sasa. Kama haitoshi, WAHADHIRI (utawala wa chuo-UDOM) wakaona form peke yake haitoshi atwangwe na-ka PhD. Sasa si tulieni kwanza mhe. Rais anajaribu kutafakari zawadi mnayostahili. Kuweni na subra jamani Dr.atatenda muujiza kwenu kwa wakati wake.
 
Nimesikia Pinda anaenda kesho UDOM kujaribu kuweka mambo sawa hadi leo wahadhiri walikiua wanaendelea na mgomo wao na inasemekana serikali imeunda kimya kimya kamati tatu kuchunguza issue hiyo. Mwenye taarifa zaidi atuhabarishe.
 
SIPATI PICHA SIKU MLACHA ANAPANDISHWA MAHAKAMANI. Uamuzi wa busara sana huo mmana wamaigeuza udom shamba la bibi.
 
safi sana tena watapishwe yote waloiba kwanza kisha waswekwe lupango
 
Hapooo ushemeji utaishia hapo hapo...no more kubebana haki ikatendeke mahakamani....waulize kwanza intelijensia inasemaje kabla kwenda mahakamani maana nae mzee wa intelijensia ni shemeji nae....brothers wote wako in trouble
 
Hapooo ushemeji utaishia hapo hapo...no more kubebana haki ikatendeke mahakamani....waulize kwanza intelijensia inasemaje kabla kwenda mahakamani maana nae mzee wa intelijensia ni shemeji nae....brothers wote wako in trouble

Duh siku hizi hata kwenda dukani hatunabudi kuuliza intelejensiya.
 
LICHA ya kuwepo kwa taarifa kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atakutana na wadhahiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, wahadhiri hao wameendelea kuchachamaa wakisisitiza kwamba subira yao imefikia ukingoni sasa wanajiandaa kwenda mahakamani kutafuta haki yao.


Wahadhiri wa chuo hicho wamekuwa katika mgomo kuingia madarasani kufundisha kwa kile wanachodai kuwa wanadhulumiwa viwango vya mishahara wanavyolipwa na serikali.

Akizungumza na Mwananchi, Naibu Katibu mkuu wa chama cha wahadhiri hao (Udomosa), Peter Kokeli alisema juhudi zao kubwa wamezielekeza katika kuhakikisha wanapata haki zao.Kokeli alisema wamekuwa na mategemea kuwa Rais Jakaya Kikwete atalitatua suala hilo lakini tayari wameanza hatua za kwenda mahakamamani.

Licha ya kuahidi kwamba wako tayari kuzungumza na Pinda, alisema suala hilo ni kosa la jinai kwa sababu wamegunduia kwamba kumekuwa na tabia ya kughushi slipu zao za mishahara.“Wahadhiri wamesikitishwa sana na taarifa hizi za uongo.

Tunapenda kuweka wazi kuwa mishahara mipya iliyoletwa chuoni ni sawa na ngazi ya mishahara iliyolipwa pia kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Kwa mfano Tutorial Assistant (PUTS 12), kwenye vyuo vyote viwili imekuwa Tsh 1,248,070/=, lakini menejimenti ya UDOM imekata mishahara hiyo.

"Wahadhiri wamebaini nyaraka za ndani ya chuo Kikuu cha Dodoma zikionyesha kuwa mishahara mipya imeletwa na kimsingi hazina makosa yoyote kwa wanataaluma,” alisema Kokeli.

Alieleza pia kusikitishwa na kauli ya Makamu mkuu wa chuo hicho Profesa Idrisa Kikula, aliposema kuwa wahadhiri wamekosa uelewa na madai yao si ya msingi, akisema kuwa kauli hiyo imelenga kuwadhalilisha, hivyo wamemtaka aiombe radhi jumuiya hii ya wanataaluma wa UDOM.

“Tunapenda kuweka wazi kuwa madai yetu ni ya msingi sana na pia ni stahiki za msingi na za kisheria. Makamu Mkuu wa Chuo ajibu hoja na si kueneza propaganda zisizo na msingi wowote” alisema KokeliLakini kwa upande wake, Profesa Kikula alisisitiza kuwa taarifa zake ni za kweli na kwamba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atakwenda chuoni hapo leo ili kutoa maelezo kamili ya madai hayo. “Kesho (leo) Waziri mkuu atakuja hapa chuoni kueleza mambo yote wanayolalamikia.

Lakini pia kuna mkaguzi wa serikali anayefanya ‘special auditing’ (ukaguzi maalum) kuanzia wizarani, atakuja hapa Jumatatu kutoa maelezo yake. Ukweli wote utajulikana,” alisema Profesa Kikula. Akizungumzia hatua ya wahadhiri hao kufungua kesi mahakamani, Profesa Kikula alionyesha kutokutishwa na hatua hiyo.

“Mahakama zipo waache waende tu. Jana nimetoa matangazo ya ujio wa Waziri Mkuu. Nimetoa pia tangazo la mkaguzi wa hesabu za serikali. Sasa kama wao wanakwenda mahakamani, mimi siwezi kuwazuia.

Taarifa zote tunazo, mimi sizungumzi tu, natumia takwimu” alisisitiza Profesa Kikula. Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kwamba Pinda akiwasili leo anatarajia kukutana na wahadhiri hao na kutoa msimamo wa serikali.Akizungumza kwa niaba ya Wahadhri hao, Peter Kokeli ambaye ni kaimu katibu wa umoja huo alisema kuwa moja ya mambo ambayo wangependa Waziri Mkuu afahamu maelezo ya ufasaha kuhusu madai yao.

Alisema kuwa wako tayari kupokea maelekezo yoyote kuhusiana na kazi yao kutoka kwa Pinda kwa kuwa wanamtambua kuwa ni kiongozi wao tena mwenye heshima lakini si katika suala la kudanganywa kuhusu malipo.
Ujio wa Waziri MKuu unaweza kuwa neema kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakimhitaji kwa muda mrefu lakini kwa upande wa wahadhiri itakuwa bado ni kilio kwani wao wanamhitaji rais mwenyewe.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Profesa Kikula, Pinda pamoja na mambo mengine anatarajia kuzungumza na wanafunzi wa UDOM pia pamoja na kukagua miradi ya chuoni hapo ikiwemo majengo pamoja na mifumo ya maji.

Kokeli alisema kuwa Wahadhiri wana mashaka kuwa suala lao ni kama moja ya vitu ambavyo Waziri Mkuu atakuwa akivijadili lakini halitiliwi uzito mkubwa kutokana na ukweli kuwa hata katika mlolongo wa mambo ya kufanya liko katika ajenda ya nne.

“Unaweza kuona ni namna gani kuwa Waziri Mkuu hakupanga kuzungumza na sisi kwani hata katika ajenda sisi tumewekwa nafasi ya nne ni kama yaliyomo, lakini tumekubaliana kwa pamoja kuwa lazima tutakutana na kiongozi wetu huenda akawa na maagizo kutoka ngazi ya juu yake lakini tutapenda atuambie lini tunalipwa pesa zetu na si vinginevyo” alisema Kokeli.

Kiongozi huyo alisema katika maombi na malengo yao wanatarajia kumuona Rais Jakaya Kikwete akiingia katika viwanja hivyo na kukaa meza moja na wahadhiri hao ili kilio chao kiweze kufika mahali panapotakiwa na kwamba uwepo wa Pinda inawezekana ukawa ni kwa ajili ya wanafunzi.

Katibu huyo alisema wamekubaliana kuiburuza menejimenti ya Chuo mahakamani kama wataona haki yao haiipatikani na wanaiomba serikali ikubali kumtuma mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Ili afanye ukaguzi wa mali za Udom ikiwemo masuala ya fedha.

Katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja kumekuwa na mfululizo wa migomo na maandamano ya wanachuo wa Chuo hicho wakishinikiza kuonana na Waziri Mkuu huku wahadhiri wao walioanza mgomo mwanzoni mwa wiki wakitaka kuonana na Mkuu wa nchi.

Dai kubwa la walimu hao ni kupunjwa kwa mishahara yao kunakofanywa na uongozi wa Udom kwa kile walichokiita kuwa ni uchakachuaji mkubwa ndani ya menejimenti ya utawala na fedha chuoni hapo.

Wahadhiri hao walisema kuwa hawana shida na Hazina kwani mishahara yao inaonyesha kuwa imekuwa ikitumwa vizuri lakini tatizo lipo ndani ya uongozi wa chuo wenyewe ambao wanashindwa kulipa mishahara kama ilivyotumwa na Hazina.

Tatizo lingine ni pamoja na kutolipwa kwa fedha za kujikimu tangu walipoajiliwa ambao wengine wanazaidi ya miaka mitatu lakini hawajui ni lini watalipwa fedha za kujikimu kama wahadhiri wa vyuo vingine.Mwisho
 
Kwa wiki nzima sasa tumekuwa tukisikia story za migomo kwa wanafunz wa kitivo cha elimu UDOM pamoja na walichokiita extended meetings kwa Wahadhiri wote wa chuo hicho kinachotarajiwa kuwa chuo kikubwa kabisa Afrka mashariki na Kati! Tatizo kubwa tumeskia kuwa ni unyanyasaji katika malipo yao,ukosefu wa vitendea kazi maofisini,n.k huku wanafunzi wakilalamikia kutorudishiwa pesa zao walizolazimishwa kulipa kabla ya kuona % zao toka Loan bodi,pesa za accomodation ziszo endana na siku halis za kuishi chuoni,mazingira mabovu ya kusomea ikiwa ni pamoja na kufurika kwa wanafunz madarasan wakati wa lectures,kukosekana kwa seminars kwa baadhi ya kozi,n.k! Ikumbukwe kuwa madai yao yanaendelea mpaka leo ambapo wanatarajia kuonana na Mizengo Pinda! "Tuombe kheri ayatolee ufumbuzi"!! Lakin pamoja na hayo, wanafunzi na wahadhiri kilio chao kikubwa ni Muhusika wa idara inayohusika na Fedha(FINANCE) Prof.SHAABAN MLACHA aachie ngazi! Sasa je, serikali kutochukua hatua mapema kunusuru masomo kwa hawa vijana ni kupuuza madai yao,kutoona umuhimu wa Elim ya wanaUDOM(Kwa vile vyuo ni vingi),walikuwa wanajipanga au walikuwa wanashughulika na mambo mengine kama ku/towalipa Dowans!?au UDOM walikuwa wanapimwa imani?? Watanzania Tujenge tabia ya kupenda Elimu kwani "Education is life in itself"(J.DEW)
 

Jamani tutasema mara ngapi kuwa sio kweli kwamba UDOM walimchangia JK pesa ya kuchukulia form? Mbona watu hawataki kuelewa? Ni propagandao hizo kwani wafanyakazi wa UDOM si wote wana CCM. Kuna mtu anasema hapo juu kuwa tulivaa hadi kofia na TShirts za CCM. Napenda niwahakikishie kuwa si kweli kwani wakati JK anakuja Dodoma kwenye kampeni mabasi yalitolwa kwa wafanyakazi kwenda kumsikiliza lakini hakun hata mmoja aliyekuwa na interest ya kwenda. Ni kweli kwamba THE TOP THREE wa UDOM ni CCM damu. Na kwenye mchakato wa kumpa mtu degree ya heshima si wafanyakazi wote wahusika, ni jopo la maprofesa wachache wa juu.
Please dont be too negative about UDOM staff
 
Wandugu samahani kwa kutowajulisha kwa muda kinachoendelea kuusu mgogoro ulipo UDOM. hivi sasa waziri mkuu yupo hapa, stay tuned.
Colgate
 
Wandugu samahani kwa kutowajulisha kwa muda kinachoendelea kuusu mgogoro ulipo UDOM. hivi sasa waziri mkuu yupo hapa, stay tuned.
Colgate

Tunasubiri kwa hamu kujua hatima ya masilahi ya wahadhili wa vijana wetu.
 
Kwanini tunakaa na kuwaendekeza watu kama hawa wanaojiita mamkwe...?wana UDOM tumeshakutambua wewe ni nani..inaonyesha watu wanaogopa tu kumtaja jina ila huyu ni Masoud..
(1)Ni TA anayekaa kwenye nyumba nzima pekee
(2)Kila siku anapingana na madai ya UDOMASA
(3)Anafundisha college ya Informatics
 

Duuu!!!!! Huyu jamaa si ndo nilisikia ni miongoni mwa ma puppet wa Mlacha. Shame on him.
 

Wewe unaejiita mamkwe. Tunakujua kuwa ww ni kibaraka wa wakubwa. Na ukiendelea kukataa nitakutaja kwa jina humu forum. Najua upo college gani na unafundisha masomo gani. Wakati wenzio wapo Chimwaga kupigania maslahi yao ww ulikuwa ukiendelea na kufundisha (Informatics). Unaona unavyojisahau na kusema "Leo nimeona tangazo linalowataka wafanyakazi wasiotaka kuendelea na sera ya mazishi wajitoe,...." Umeona tangazo hilo ukiwa wapi? Unguja? Kwa kuwaweka wazi wana JF, tangazo hilo limetoka na kubandikwa mbao za matangazo hapa UDOM. Kwa maana hiyo mtu aliyekuwa nje ya UDOM hawezo ona hilo tangazo.
Wewe msaliti mamkwe tunakutambua na tukimaliza kuwashughulikia hao wakubwa zako tunakuja kwako informal
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…