Kwa ufahamu wangu mgomo wa Waalim uko siku nyingi, ila nadhani bado tu kutangaza kwa vinywa vyao au maandamano. Tofauti ya mgomo wa Madaktari na Waalim ni immediate impact ya mgomo, Madaktari wakigoma basi wagonjwa hufa ndani ya masaa 24 au baadaye kidogo tu, lakini walimu wakigoma basi impact yake utaikuta katika matokeo ya form four. Kwa takwimu za Wizara husika kwa miaka miwili iliyopita matokeo ya form four kwa division I-III imekuwa ni asilimia chini ya 15% ya watahiniwa wote na hawa ndiyo tunawategemea waende form five na hatimaye vyuo vikuu na division iv-O ni zaidi ya 84% ya watahiniwa wote! Kwa sisi waelewa wa tasnia ya elimu hiyo asilimia 84 ambao hawana uwezo wa kuendelea na shule na hata vyuo wakati mwingine hilo ni bomu litakalo lipuka wakati wowote.