Mgomo waingia siku ya 3 Chuo Kikuu St. Joseph

D 2de A

Senior Member
Joined
Jun 7, 2013
Posts
183
Reaction score
32
Wanafunzi St.Joseph wagoma kuingia darasani



NA SHAABAN MDOE,ARUSHA
ZAIDI ya wanafunzi 350 wa Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Joseph, tawi la Arusha, wamegoma kuingia madarasani kwa madai ya kufundishwa kwa mitalaa kutoka nchini India.

Mbali na hilo, wanafunzi hao ambao wanasomea ualimu, wanadai kufundishwa na walimu wenye fani ya uhandisi na kwamba huimbishwa nyimbo za darasa la kwanza, pili na tatu.

Kiongozi wa Chuo hicho, Bwigane Mwaipaja, alisema tokea mwanzo wa muhula wa masomo, walibaini kuwepo kwa mitaala tofauti katika chuo hicho.
Alisema chuo hicho kinatofautiana na vyuo vingine kutokana na kufundishwa kwa kutumia mitaala kutoka nchini India, ambayo haiendani na mitaala ya Tanzania.

Mwaipaja alisema wanafunzi hao hawafundishwi masomo ya vitendo, badala yake wanafundishwa kuimba nyimbo za darasa la kwanza, pili na tatu.
Alisema mapungufu mengine katika chuo hicho ni kwamba wanafunzi wanafundishwa na walimu wenye fani ya uhandisi, ambao hawana taaluma ya ualimu.

Mwaipaja alisema baada ya wanafunzi kubaini kasoro hizo, waliwasilisha malalamiko yao katika uongozi wa chuo hicho, ambao uliahidi kulipatia ufumbuzi muhula wa pili wa masomo utakapoanza, lakini halikupatiwa ufumbuzi.
Alisema walizungumza na walimu wao ambao walidai hawana taaluma ya kufundisha masomo ya ualimu.
Mwanafunzi Rehema Swai, alisema mtaala huo wa India hauna muhuri kutoka TCU na kwamba wanaiomba serikali itoe tamko iwapo mtaala huo unafaa kufundishwa nchini.

Kwa mujibu wa Rehema, hulazimishwa kutafuta manyoya ya kuku au ndege na kuyagandisha kwa gundi katika madaftari ya somo la mazoezi, tofauti na vyuo vingine.

Alisema elimu wanayopatiwa chuoni hapo ni sawa na kupoteza muda na fedha na kwamba hawawezi kuitumia sehemu yoyote.
Mwalimu msaidizi wa chuo hicho, Josephat Tambu, alikiri kuwepo kwa malalamiko ya wanafunzi hao ambapo alisema suala hilo linahitaji muda kutatuliwa.

Alisema chuo hicho hakina uhaba wa walimu na kwamba tatizo la kuwepo kwa walimu wasio na uwezo litapatiwa ufumbuzi baada ya muhula wa masomo kumalizika.


CHANZO: Uhuru
 
Wahindi ni majanga nchi hii. Turudi kwa IMTU
 
hao jamaa ni wazuri katika uhandisi na sio uwalimu,poleni sana jamani...
 
Jana ilikuwa ni siku ya tatu toka wanafunzi wa St Joseph kugoma, wakidai curriculum mbovu ya chuo ilekebishwe kisha wapewe prospector. Uwezekano Mkubwa uliopo ni chuo kufungwa kwa muda usiojulikana.
 
Sio hayo tu mkuu laboratory Zenyewe tulizonazo pale ni kama za st kayumba hakuna vifaa vya kutosha. Watu tunafanya practical bila any theory about topic. Isitoshe practical Zenyewe toka form one nmefanya
 
mh poleni mngeenda tawi la dar wako vizuri pale.
 
Maua mazuri yapeendeeza..Maua mazuuuri yapeendeeza..Ndio michezo hii wanafanya? Wahuni hawa, gomeni tu.
 
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Vyuo vikuu vyetu havina mitaala. Juhudi ndo zinafanyika sasa ili kuwepo mitaala hiyo. Na wanafunzi tunajua kazi ya mitaala? Mitaala mingi ikiwapo inaandaa wanafunzi kuajiriwa mara wanapohitimu masomo yao.

Shida za maabara zipo hata katika vyuo vikongwe kama UDSM na SUA. Kuwa na maabara ni kitu kimoja na vitendanishi katika maabara ni kitu kingine na achilia mbali wataalamu katika maabara husika.

Ushauri wangu kwa wanafunzi hawa, wasipoteze muda wao kwani dakika moja iliyopotea huwa hairudi. Waende wakajiunge chuo kingine chenye mitaala. Yaani nguvu ya hela yao ifanye kazi hapa kuliko kupoteza muda kwa migomo.

Swali la kujiuliza, watanzania wanaoenda kusoma nje ya nchi yetu, ambao ni wengi, huwa wanasoma kwa mitaala ya Tanzania?
 

Yani umeanza na porojo ila umemaliza with a logical question mkuu
 
Yani umeanza na porojo ila umemaliza with a logical question mkuu

Mkuu, wanaosoma Biblia; wanasema kila neno lililomo katika kitabu hicho lina mwenyewe. Na katika ujumbe wangu naamini kuwa kila neno lina mwenyewe. Nakushukuru wewe kwa kukiri kuwa neno la mwisho limekugusa (ndio lako) na mengine kwako ni porojo. Asante
 
Poleni!
But msipoteze mda wenu bure, tafuteni vyuo vingine vinavyoeleweka kuliko kugoma na mpaka hilo swala lije litatuliwe lita take a long time!
 
Hivi vyuo vya kuokoa jahazi kwa wale ambao maksi zao "hazikutosha" vina shida sana
 

Tatizo ni kwamba mtaala umefanyiwa editing kutoka kwenye mtaala wa engineering, vile vile wakufunzi ni maengineer na sio waalimu(teachers). Kwa hiyo mtaala haukuthibitishwa na TCU, vile vile kwa mujibu wa NACTE ukihitimu kwa mtaala huo haupati cheti wala kuajiriwa sehemu yoyote.
 
Dah......! Poleni sana wana St.Joseph, lakini mungu yupo kwa huo uhuni waliowafanyia hao wahindi, ila mkae mkijua ridhiki la mtu halizuiriwi na mwanadamu isipokua tu anaweza akakucheleweshea, so iz better mkaaply vyuo vingine kuliko kukaa apo na kupoteza muda wenu hao jamaa wapo kibiashara zaidi so kuweni makini sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…