Taifa ni watu. Taifa fulani linapokuwa maskini au tajiri huashiria umaskini au utajiri wa Taifa hilo. Uchumi wa nchi unapokua au kuanguka humaanisha uchumi wa wananchi wa nchi hiyo unakua au kuanguka.
Nchi yetu imejaliwa kila kitu chema lakini tumenyimwa super intelligent leaders. Yaani ukiangalia, kwa kiasi kikubwa, vuongozi wana low IQ kwa kiasi kikubwa kuliko baadhi ya wananchi wanaowaongoza. Hapa ina maana kipofu amepewa kazi ya kumwongoza anayeona.
Serikali imetangaza kuwa ukuaji wa uchumi wa Taifa umeanguka (kwa mwenye akili, hiyo inaashiria kuwa ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja umeporomok).
Kama uchumi wa mtu mmoja mmoja umeporomoka, na kama kiongozi una akili, utawezaje kumbebesha mzigo zaidi wa tozo mwananchi ambaye tayari uchumi wake upo taabani? Bei kubwa ya diesel inasababishwa na Serikali. Karibia 50% ya bei ya mafuta, yote ni kodi na tozo za Serikali na taasisi zake. Imeona hiyo haitoshi, ikaamua kuweka tena tozo ya sh 100 kwa kila lita. Kama una lori ambalo linalotumia lita 100 kwa siku, ina maana umeongezewa sh 300,000 kwa mwezi. Halafu kuna afisa mjinga huko huko kwenye mamlaka za Serikali anasema hajui kwa nini bei ya gas imepanda. Hivi hiyo gas inasafirishwa kwa nyungo kuweza kumfikia mteja?
Mataifa karibia yote yanayoongozwa na viongozi wenye akili na weledi, kutokana na kuporomoka kwa uchumi wa wananchi wao, wamejitahidi kuondoa tozo mbalimbali na kupunguza kodi ili wananchi wapate unafuu wa namna fulani kutokana na vipato vyao kuyumba kutokana na janga la corona. Sisi hapa kwetu, Watanzania wakazawadia tozo ya miamala! Yaani mgonjwa ambaye kuubeba mwili wake tu ni tatizo, sasa anabebeshwa LUMBESA.
Hakika, katika vitu vyote vilivyo muhimu katika kuleta maendeleo ya Taifa, cha kwanza, na muhimu kuliko vyote, ni uongozi wenye weledi, maono na ubunifu. Lakini, kwa bahati mbaya mkiwa na uongozi kama huu wa Serikali yetu, hata mpewe nini, mtaendelea kuwa maskini. Maana ni Serikali ya kudidimiza badala ya kuwa serikali ya kuwezesha na kusaidia. Ni serikali ya kuleta huzuni na masikitiko badala ya kuwa serikali ya kuleta furaha na matumaini.
Taifa lipo kwenye mtihani mkubwa. Kitendo cha CCM kukumbatia watu waongo, wanafiki, wenye uelewa mdogo na wasio na maono wala weledi kunaligharimu sana Taifa. Leo ni vigumu sana ndanibya CCM kumwona mtu ambaye ni super itelligent, mkweli wa nafsi, maneno na vitendo, mwenye weledi na maono. Wamejaa wanafiki na wapiga porojo, halafu tunatarajia eti hao watupeleke kwenye maendeleo. Hakika tunasubiria samaki chini ya mbuyu.
Leo tuna Serikali ambayo kazi yake kubwa ni kuua uchumi. Wao wanachofanya ni kuhakikisha kila mwenye kuanza kumea kiuchumi, anafia pale pale anapoota. Ndiyo maana mtu akienda kuomba leseni ya biashara, hajauza chochote, wanataka alipe kodi, wanataka afe kibiashara, kabla hajaanza biashara. Sijui ni kodi ya nini maana msingi mkuu wa kodi, ni kulipa kiasi fulani kutoka kwenye faida unayoipata kutokana na biashara au uwekezaji wako.