Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Leo tarehe 15/03/2020 nilimuwakilisha Mh Mbunge wa Mbeya Mjini #JOSEPH #OSMUND #MBILINYI(SUGU) kumjulia hali dada #Rosemery #Mayemba mkazi wa mtaa wa Ilolo kata ya Sinde na kumpatia pesa kwaajili ya nauli na pesa ya kujikimu wakati atakapokua Dares salaam Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako hana ndugu yeyote.
Siku tatu zilizopita video ya Rosemery ilisambaa ikimuonyesha yeye na mtoto wake wa kiume (miezi 2) aliezaliwa na uvimbe usoni akiomba msaada wa matibabu .
Baada ya Mh Mbunge kupata taarifa hizo kwa njia ya mtandao tulimfuatilia na kugundua alishapewa rufaa ya kwenda Muhimbili na kwa bahati mbaya akakutana na changamoto ya nauli na pesa ya kujikimu akiwa huko,tatzo hili limeshughulikiwa leo na kesho tarehe 16/03/2020 atakua njiani kuelekea kwenye matibabu Dares salaam.
Siame g.k
Katibu wa Mbunge.
Nimeona hili bandiko kuwa dada Rosemary anaeuguliwa na mtoto wake, amepata rufaa kwenda Muhimbili lakini alikosa nauli na pesa za kujikimu ilhali hana ndugu Dar.
Afrika familia ndiyo safety net ukiwa na matatizo lakini hili ni jukumu la idara ya ustawi wa jamii kusaidia wenye mahitaji kama ya dada Rosemary.
Tunamshukuru sana mheshimiwa Sugu kwa kitendo chako cha ukarimu kuamua kumsaidia dada Rosemary. Inawezekana hakuwa anafahamu nani wa kumuona mpaka ameamua kutoa shida yake kwenye mitandao ya kijamii.
Yule aliyemuandikia rufaa ya kwenda Muhimbili alifahamu kuwa bila msaada wa pesa ile rufaa haikuwa na maana? Alipaswa kwanza kuwasiliana na afisa ustawi wa jamii kufahamu ni jinsi gani wangemsaidia mgonjwa huyu.
Hiyo ndiyo inaitwa holistic assessment. Huangalii ugonjwa tu wa mgonjwa unaangalia pia matatizo yanayomzunguka mgonjwa ambayo yakitatuliwa yataharakisha uponaji.