OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Mimi sijazama sana kwenye biblia na neno la Mungu.
Nina jirani yangu hapa mdogo wake anaumwa masuala ya uzazi na vidonda vya tumbo. Ana hali ngumu sana kiafya na safari za Bugando haziishi. Pamoja na madaktari Dada jirani amekuwa na option ya kwenda mchungaji kuombewa na kukabidhi swala lake kwa Mungu amponye.
Watu hawa nawaonea huruma sana kwa sababu hawana bima na matibabu ni ghali.
Sasa mchungaji amewashauri wamtolee sadaka Mungu ili awaponye. Amesema ni sadaka ya nathiri wamtolee sana Bwana na wamuombe awaponye. Mchungaji amewasihi wasisite kumtolea Bwana kama wafanyavyo hospitali.
Hii imekaaje wakuu. Maana hawa ndugu wanapambana kupata fedha ya matibabu halafu tena sadaka?!
Tujadili bila kashfa wala matusi. Ni kwa hoja tu