Mgonjwa mwingine wa Ebola afariki Uganda

Mgonjwa mwingine wa Ebola afariki Uganda

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mgonjwa mwingine ambaye ni mtoto mdogo, amefariki kwa Ebola katika hospitali moja katikati mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa taarifa za gazeti la New Vision la nchini humo.

Maafisa wa afya wanasema kuwa marehemu alikuwa mmoja wa watu 14 waliolazwa hospitalini wakiwa na dalili kama za Ebola. Uchunguzi pia unafanywa kwa watu sita waliofariki kutokana na kile wenyeji wamekitaja kuwa ugonjwa wa ajabu mapema mwezi huu.

Siku ya Jumanne, Shirika la Afya Ulimwenguni lilithibitisha mlipuko wa kwanza wa ugonjwa wa Ebola nchini Uganda ikiwa kwa zaidi ya muongo mmoja tangu ugonjwa huo utokee nchini humo.
 
Back
Top Bottom