Mgonjwa wa Ukimwi yupo katika stage ya mwisho naombeni ushauri

Mgonjwa wa Ukimwi yupo katika stage ya mwisho naombeni ushauri

Status
Not open for further replies.

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2018
Posts
11,936
Reaction score
15,196
Wadau nianze kwa kuwapa pole za mihangaiko ya kutwa mzima ya leo.

Nina ndugu yangu anaumwa ngoma yupo stage ya mwisho. Amepelkwa hospital nyingi kila hospital unapiga rufaa kwenda hospital nyingine kama vile hataki field pale.

Hali imekuwa mbaya zaidi maana hali, hatembei na ametokwa na vidonda mdomoni na kooni mwili umedhoofu sana. Wajuzi wa mambo tumsaidie ndugu yangu huyu kama kuna Tiba yeyote hata Tiba mbadala.

Note ameshaacha dawa ARV

Karibuni kwa michango yenu.

MREJESHO
Nawashukuru.
Mgonjwa ameshafariki. Ubarikiwe sana
 
Poleni sana mkuu, ngoja waje wataalam wa tiba naimani watakupa muongozo zaidi
 
Kuna nchi zimepitisha Sheria za 'kumrestisha in peace' mgonjwa ambaye anaaminika hawezi kupona, ambapo Yeye au (na) ndugu Wana 'sign' form maalumu sijui kwa nchi za Africa.

Cha msingi ni kumuombe tu kwa Mungu unayemuamini.!
 
Kuna ukweli Mchungu nlitaka kuusema lakini si vizuri..!! Pole sana ndugu yangu lakini USIJARIBU KUACHA DAWA ZA UKIMWI yani hata ukijakuziirudia ulizoiacha unakuta hazifanyi kazi virus washakuwa suguu.. Wengi huwa hawaponiii.
na mimi nilitaka ninyooshe maelezo na hisi hivyo ulivyofikiri lakini nikaona ngoja ni replay hivyo tu inatosha
 
Kosa kubwa sana ndugu yako alilofanya ni kuacha dawa, na wengi huwa wa naacha kumeza ARV kwa kudanganywa na maombi, mtu akisikia ushuhuda kanisani kwamba watu wanaombewa wanapona nae anaamini, nenda kwenye maombi lakini dawa usiache ndugu.
 
Kwa maelezo yako huyo ameshatoka kwenye stage ya HIV sasa hivi yuko kwenye stage ya AIDS which is no reversible.

Labda kwenye vituo vya HIV research labs wangeweza kumpa combination ya ARVs kupitia mishipa ya damu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom