Mgunda, nakushauri beba waganga wote wa kienyeji Tanga, Jumapili hamna mpira ni mauza uza tu

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Mimi nimeanza kwenda kushuhudia mechi za Simba vs Yanga mwaka 1989 wakati marehemu John Makelele Zig Zag anatunusuru tusishuke daraja baada ya uzembe wa kipa marehemu Sahau Said Kambi. Mechi hizi kama wageni wa soka watakufa bure kwa presha, timu lenyewe tumeliona kule Sudan halina mpira wowote zaid ya maneno tu, sababu kibao eti mazingira hayakuwa mazuri, shenzi kabisa.

Nakushauri mdigo mwenzangu Juma Mgunda, nimekuona mwenyewe ukicheza soka pale Coastal Union, enzi hizo golini marehem Hamis Makene, kulia Said Kolongo, kushoto Douglas Mhani, nne Yassin Abuu Napili, tano marehem Idrisa Ngulungu mguu mfupi, sita Ally Maumba over the top, winga Kassim Mwajeki, winga Razack Yussuf, nane Kassa Mussa, tisa wewe Juma Mgunda na kumi Hussein Mwakuruzo.

Nisikilize Mgunda, jamaa zetu wanatamba tarehe 23 wanakwenda kupoteza machungu siyo kwa uwezo dimbani, ni mambo nje ya uwanja, watapitia milango mingine na kila aina ya fujo, fanya kama alivyokuwa akifanya marehemu Mansour Magram wakati akifundisha Sigara.

Yanga hawakuwahi kumfunga Sigara ya Magram, alichezesha wachezaji wababe tu akina Rashid Mmanga, Shaban Anania n.k. Alipokuja Simba pia, Magram kila mchezo na Yanga namba sita Simba lazima acheze Marehemu Idd Seleman kibode, Bakar Idd n.k, na wewe weka wahuni tu.

Sasa hivi jamaa wameanza kutafuta wadudu na wanyama wa kuroga, Tanga ndiyo kwetu mambo hayo, nenda Duga, nenda Mwahako, nenda Mwakidila, nenda Mabokweni ndiyo balaa, wakusanye wape kazi. Ukimfunga Yanga umekula mkataba mnono baba.

Enyi wadigo wenzangu tumsaidie Mgunda katika hili, wadigo hatushindwi kitu sisi.

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
 
Jamaa kabeba toka Sudan

images (3).jpeg
 
Hofu tayari imeshatanda kwa team makolo kuelekea hiyo tarehe 23! Wakikumbuka ya nyuma, wanatamani kama mechi iahirishwe vile.

Maana furaha yote ya kuwafunga wale vibonde kutoka Angola, itayeyuka ghafla.
 
Tuseme tu ukwel Simba anazidiwa na yanga nje ya uwanja tu .kimpira hasa mpira wa kimkakati yanga bado Sana kwa Simba .
Dawa ya Moto ni Moto ,umafia juu ya umafia na weekend hii tukiwapiga nakwambia watapoteana Hawa watu na kuanza kufukuzana hovyo .
Kizur Zaid hii game Sina waswas nayo kabisa ,means tunashinda Tena goli mbili na kuendelea .
 
Simba inapaswa iindeleze furaha tuliyonayo wanasimba tuliyoipata kuanzia jana mpaka hiyo tar 23. Mgunda tunakuaminia
 
Endeleeni kujitekenya na kucheka wenyewe, mmeota mapembe baada ya kuifunga ihefu ya angola na kuanza kulinganisha ubora wa kikosi cha yanga na cha kwenu, kweli Rage akukosea, kuondolewa kwa yanga klabu bingwa aiondoi ubora wa kikosi walichonacho na mkiingia na iyo mentality ya kwamba mmekuwa bora kwa kuifunga ile ihefu ya angola mtaondoka uwanjani kabla mpira aujaisha nawapa angalizo wekeni akiba ya maneno mtafurukuta kwa wengine na sio kwa yanga nawapa taadhali
 
Mimi nimeanza kwenda kushuhudia mechi za Simba vs Yanga mwaka 1989 wakati marehemu John Makelele Zig Zag anatunusuru tusishuke daraja baada ya uzembe wa kipa marehemu Sahau Said Kambi. Mechi hizi kama wageni wa soka watakufa bure kwa presha, timu lenyewe tumeliona kule Sudan halina mpira wowote zaid ya maneno tu, sababu kibao eti mazingira hayakuwa mazuri, shenzi kabisa.

Nakushauri mdigo mwenzangu Juma Mgunda, nimekuona mwenyewe ukicheza soka pale Coastal Union, enzi hizo golini marehem Hamis Makene, kulia Said Kolongo, kushoto Douglas Mhani, nne Yassin Abuu Napili, tano marehem Idrisa Ngulungu mguu mfupi, sita Ally Maumba over the top, winga Kassim Mwajeki, winga Razack Yussuf, nane Kassa Mussa, tisa wewe Juma Mgunda na kumi Hussein Mwakuruzo.

Nisikilize Mgunda, jamaa zetu wanatamba tarehe 23 wanakwenda kupoteza machungu siyo kwa uwezo dimbani, ni mambo nje ya uwanja, watapitia milango mingine na kila aina ya fujo, fanya kama alivyokuwa akifanya marehemu Mansour Magram wakati akifundisha Sigara.

Yanga hawakuwahi kumfunga Sigara ya Magram, alichezesha wachezaji wababe tu akina Rashid Mmanga, Shaban Anania n.k. Alipokuja Simba pia, Magram kila mchezo na Yanga namba sita Simba lazima acheze Marehemu Idd Seleman kibode, Bakar Idd n.k, na wewe weka wahuni tu.

Sasa hivi jamaa wameanza kutafuta wadudu na wanyama wa kuroga, Tanga ndiyo kwetu mambo hayo, nenda Duga, nenda Mwahako, nenda Mwakidila, nenda Mabokweni ndiyo balaa, wakusanye wape kazi. Ukimfunga Yanga umekula mkataba mnono baba.

Enyi wadigo wenzangu tumsaidie Mgunda katika hili, wadigo hatushindwi kitu sisi.

Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
Mabokweni ndiobalaa????? Mkuu uliza tukua.bie waganga wako wapi
 
Back
Top Bottom