Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 390
- 1,425
Mimi nimeanza kwenda kushuhudia mechi za Simba vs Yanga mwaka 1989 wakati marehemu John Makelele Zig Zag anatunusuru tusishuke daraja baada ya uzembe wa kipa marehemu Sahau Said Kambi. Mechi hizi kama wageni wa soka watakufa bure kwa presha, timu lenyewe tumeliona kule Sudan halina mpira wowote zaid ya maneno tu, sababu kibao eti mazingira hayakuwa mazuri, shenzi kabisa.
Nakushauri mdigo mwenzangu Juma Mgunda, nimekuona mwenyewe ukicheza soka pale Coastal Union, enzi hizo golini marehem Hamis Makene, kulia Said Kolongo, kushoto Douglas Mhani, nne Yassin Abuu Napili, tano marehem Idrisa Ngulungu mguu mfupi, sita Ally Maumba over the top, winga Kassim Mwajeki, winga Razack Yussuf, nane Kassa Mussa, tisa wewe Juma Mgunda na kumi Hussein Mwakuruzo.
Nisikilize Mgunda, jamaa zetu wanatamba tarehe 23 wanakwenda kupoteza machungu siyo kwa uwezo dimbani, ni mambo nje ya uwanja, watapitia milango mingine na kila aina ya fujo, fanya kama alivyokuwa akifanya marehemu Mansour Magram wakati akifundisha Sigara.
Yanga hawakuwahi kumfunga Sigara ya Magram, alichezesha wachezaji wababe tu akina Rashid Mmanga, Shaban Anania n.k. Alipokuja Simba pia, Magram kila mchezo na Yanga namba sita Simba lazima acheze Marehemu Idd Seleman kibode, Bakar Idd n.k, na wewe weka wahuni tu.
Sasa hivi jamaa wameanza kutafuta wadudu na wanyama wa kuroga, Tanga ndiyo kwetu mambo hayo, nenda Duga, nenda Mwahako, nenda Mwakidila, nenda Mabokweni ndiyo balaa, wakusanye wape kazi. Ukimfunga Yanga umekula mkataba mnono baba.
Enyi wadigo wenzangu tumsaidie Mgunda katika hili, wadigo hatushindwi kitu sisi.
Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app