Mguu kwa Mguu Vita ya Kiuchumi Sehemu ya kwanza

LAZIMA NISEME

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2015
Posts
240
Reaction score
267
MAADUI WA VITA YA UCHUMI

Waraka wa BASHIR YAKUB.
+255784482959.

SIKILIZA Radio CHANYA

Tumegusa uchumi wa bepari. Mara zote, na kote duniani bepari alipoguswa kwenye uchumi wake basi ametumia mbinu hizi hapa chini kuhakikisha anapambana na waliomzuia.

[a] Kumwita kiongozi anayeongoza vita ya uchumi Mvunjaji wa haki za binadamu na asiyefaa. Imetokea kwa Gaddafi baada ya kumnyima bepari mafuta, halikadhalika kwa Saddam Hussein.

Pia ndilo tatizo la Mugabe na bepari baada ya kurudisha mashamba kwa wazawa ili wafaidi uchumi wao.

Kuratibu na kufanikisha matukio ya ajabu kwenye jamii ili kuleta faraka,taharuki, chuki, uadui, na sintofahamu.

Bepari analiweza sana hili hasa nchi za Afrika kutokana na uwezo wake mkubwa wa fedha na teknolojia.

Lengo la mbinu hii ni :
Kuwatoa kwenye ajenda ya vita dhidi yake na kuwaelekeza kwenye mijadala mingine.
Kuchonganisha watu, serikali na viongozi wao.
Kupeleka ujumbe duniani kuwa kiongozi fulani na serikali yake hawafai tena.
Kuligawa taifa kati ya upande unaoamini matukio kutekelezwa na fulani na upande unaoamini vingine.

[c] Kuandaa mapinduzi kwa kuwatumia wasaidizi wa rais na viongozi wenye tamaa.

[d] Kuandaa maandamamo makubwa ambayo mwisho wake ni kuuondoa utawala uliodhibiti uchumi .

Utaona waandamanaji wanalalamika kuchoshwa na mambo mbalimbali lakini kumbe nyuma yao ni fedha, mbinu na mipango ya bepari.

Bila hata waandamanaji kujua isipokuwa wachache/viongozi wao. Mbinu hii imetumika hivi karibuni kuondoa viongozi wengi wa Afrika ya Kaskazini waliodhibiti uchumi wao kwa mda mrefu.

[e] Kufadhili makundi ya waasi Mf. Congo, Sudani Kusini, Sierra Leone, Liberia nk.

Badala ya kujadili udhibiti wa rasilimali zenu mnajadili amani itapatikana vipi huku bepari akitumia nafasi hiyo kuiba.

[f] Kufadhili na kuviimarisha vyama vya upinzani hasa vyenye tamaa ili hatimaye na kwa namna yoyote ile viondoe madarakani viongozi waliombana bepari.

[g] Kutafuta sababu na hatimaye kuweka vikwazo vya kiuchumi.

Lengo ni kuwafanya wananchi wapate taabu ili wachoshwe na utawala uliombana bepari na hivyo kufanya maamuzi ya kuuondoa kwa namna yoyote. nk, nk, nk............

NINI MFANYE KTK KIPINDI KAMA HIKI.

[a] Kushikamana na kutokubali kutenganishwa kwa matukio.

Kutokuwa na majibu ya haraka ktk mambo makubwa.

[c] Vyombo vya usalama kujiimarisha kiulinzi na kuhakikisha vinafika kwenye majibu ya mzizi wa kila tukio na kutoa taarifa kwa wakati kwa umma.

[d] Vyombo vya usalama kutokubali kusaidiwa upelelezi na nchi za mabepari kwakuwa mwanya huo hutumika kutoa majawabu aidha yanayo divert ukweli au yanayokamilisha malengo yaliyokusudiwa.

[e] Kuepuka kabisa kuchanganya tofauti zetu za kisiasa za tokea huko nyuma na yanayotokea sasa.

YAPI MADHARA YA KUTOSHIKAMANA KIPINDI KAMA HIKI.

Bepari hana hasara, wenye hasara ni mimi na wewe. Mpango wa wagawe uwatawale "divide&rule" haikuishia kwenye ukoloni. Bado ungalipo.

Kama tutakubali kugawanywa na majaribu ya bepari , sawa na tugawanywe tu , ila ahadi ni hii kuwa kila mmoja ataonja joto la jiwe.

Wewe uliyekubali kugawanywa utaonja na ambaye hakukubali ataonja. Mtaona Iraq na Libya aliyeshiriki na ambaye hakushiriki wote wanaonja.

Tunawasifia Angola na Botswana kwa kumbana bepari na hatimaye kufaidi rasimali zao.

Lazima tujue wamefikia hapo baada ya kushikamana na kuzishinda hila, fisadi, fitna,na mitihani ya bepari. Na sisi tunaweza.

TUTARAJIE MATUKIO ZAIDI.

Matukio bado , huu ni mwanzo tu. Hivi mlitarajia bepari abanwe halafu tubaki salama. Haiwezekani. Historia inakataa jambo hilo. Bepari lazima akutingishe.

Kama ingekuwa tumbane bepari halafu tubaki
salama basi isingeitwa Vita ya Uchumi bali Sherehe/tafrija ya Uchumi. Hii ni vita na sasa mnaweza kuanza kuona taswira ya vita yenyewe.

Vitimbi na matukio yatakuja mengi. Lengo ni moja tu , kuua vita hii ili bepari aendeleze alikoishia.

Msishangae wakaanza kudhuliwa hata wanaoonekana wana mtazamo tofauti na mwenyekiti ndani ya chama tawala ili chama kigawanyike na hatimaye serikali igawanyike.

Kwa kufanikiwa kukigawa chama kinachotawala bepari anajua atakuwa amefanikiwa kuigawa serikali.

Ukifanikiwa kuigawa serikali maana yake bepari amepunguza kasi ya vita dhidi yake lakini maana yake pia anakaribia kumwondoa kabisa adui aliyebana uchumi wake.


***Tuliombee taifa letu la Tanzania wanafiki wote washindwe na hiyo vita tuishinde maana kwa Mungu hakuna lisilowezekana. Tushikamane na tutende yote kwa hekima na busara. Adui wetu atashindwa. Tunayaweza yote katika yeye atutiaye nguvu.
 
Baba "J" si amesema kuwa yeye hashauriki? Aendelee kupambana tu kivyake! Kama ni kuwagawa wananchi, Baba "J" anaongoza, tusiwasingizie hao "Mabepari," kinachotutafuna kimo humu humu ndani!
 

Safi sana mkubwa umeeleweka
 

Gaddafi na Mugabe hawana cha kuiga. Watabaki kuitwa ma-dictator.

Wananchi tuungane dhidi ya Nani?
Vita ya Kiuchumi, tunapigana na nani?

1. Na walisaini mikataba mibovu?

2. Wakina Lisu( wanasiasa)

3. Chadema

4.Maraisi wastahafu

5. Wageni(bepari)

6.Viongozi wa CCM?
 
Umekosea jukwaa.
Peleka jukwaa LA siasa maana umetumwa kutia watu uoga.
Pole !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…