Mguu unamtesa mama yangu, Msaada please

Mguu unamtesa mama yangu, Msaada please

madameA

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
435
Reaction score
176
Habari ya humu ndani wadau.

Ninahitaji msaada wa haraka kutoka kwa yeyote anayeweza nisaidia ikiwemo mawazo. Mama yangu ana miaka 70 sasa. Kama miaka 3 iliyopita alifanyiwa operation ya goti MOI akawekewa vipandikizi.

Lakini vilikataa mguu ukaanza kuota majipu. DR. wake akamwambia ana allergy hivyo inabidi arudie hiyo operation abadilishe hivyo vipandikizi. Akafanyiwa Operation mara ya pili lakini tatizo likaendelea.

Akafanyiwa Operation mara ya tatu wakamkata nyama + wakakwangua mifupa kutoka sehemu ya mwili wake wakamuwekea kwenye mguu, hapo kidogo mguu ukawa unaendelea vizuri. baada ya operation ya mara ya 3 alikaa kama mwaka 1 hivi, tukajua tatizo limeisha.

Kipindi hicho chote alikuwa ana-attend clinic kila baada ya miezi 2 lakini dr wake akawa anamwambia mguu unaendelea vizuri na alikuwa hapewi dawa ya aina yoyote.

Kama miezi 2 iliyopita mguu ukafumuka kidonda kikaanza upya kama ilivyokuwa kwanza. Inawezekana mguu ulikuwa umepona juu tu ndani ulikuwa bado mbichi.

Tukampelekea hospital (MOI) akafanyiwa mara ya 4 operation wakamuwekea 'cement' wataalamu mtakuwa mnaijua. sasa alivyotolewa nyuzi ile cement ikawa inaonekana kwa juu. leo ameenda kufunga kidonga nurse wakati anamsafisha ile cement ikatoka. kwa hiyo pamebaki shimo la kidonda.

naomba msaada wa mambo yafuatayo:

(1) Sitaki mama afanyiwe operation tena kwani kutokana na umri wake naona anateseka. hivyo naomba kama kuna ambaye anafahamu dawa ambayo anaweza akawa anatumia ili tu kidonda hicho cha operation kipone bila kufanyiwa tena operation.

(2) inaonekana Dr. amechemsha, naomba kama kuna mtu anayefahamu dr mzuri wa mifupa anielekeze na jinsi ya kumpata.

(3) ushauri mwingine wowote ambao utasaidia kwenye tatizo hili naupokea.

Aksante.
 
Pole sana,.

Jaribu kumtafuta Specialist wa mifupa (Orthopaedist), huenda tatizo likawa solved inavyotakiwa!!
 
Kama MOI imeshindikana sidhan kama sehem nyingine wanaweza kumudu kulitatua vilivyo kwa tanzania.
Tafuta suplinents zinaweza kumsaidia kupona kidonda haraka zaidi
Ukihitaj ni pm
 
Kama MOI imeshindikana sidhan kama sehem nyingine wanaweza kumudu kulitatua vilivyo kwa tanzania.
Tafuta suplinents zinaweza kumsaidia kupona kidonda haraka zaidi
Ukihitaj ni pm
Suppliments zipi mkuu. Niandikie plse.
 
Back
Top Bottom