Kuumwa mguu ni dalili ya ugongwa na wala sio ugonjwa.Tatizo linaweza kutokana na magonjwa ya jumla ya mwili au gonjwa kwenye mguu peke yake.Na inapokuja kwenye mguu, tatizo linaweza kuwa kwenye mifupa au misuli na nerva(soft tisue).Xray haina uwezo wa kuonyesha tatizo nje ya mifupa.Hivyo basi nendeni kwenye hospitali yenye madaktari bingwa(Orthopedic surgeons) ambao watachukua historia ya tatizo, watampima na baadae kumwandikia vipimo mbalimbali(Ikiwemo MRI kama ipo) kujua tatizo hasa ni nini, na atapatiwa tiba stahili.