Afrikasana
JF-Expert Member
- Oct 27, 2021
- 320
- 288
Kupitia bunge la 12,wabunge waliowengi wanampongeza waziri wa TAMISEMI Mh. Innocent Bashungwa kwa uwajibikaji na usikivu wake. Wamesema anasikiliza na kufikika kirahisi. Nampa hongera kwahilo.
Bashungwa usibweteke maana wapo baadhi ya watumishi ndani ya wizara yako bado ni majipu.
Mfano akichangia bungeni hapo mbunge wa Makete mh. Sanga amedai kwamba kiasi cha shs 222 bilioni hakijarejeshwa serikalini. Ameenda mbali zaidi akidai walengwa wa mikopo hiyo hawapewi bali wanajikopesha viongozi wahuni. Anadai viongozi na watumishi wahuni wamejitwalia fedha hizo hivyo wabanwe wazirejeshe zifanyie shuhuli za maendeleo. Kwamantiki hiyo Bashungwa fukiza moshi wahuni hao watoke mapangoni.
Jambo lingine ninalokudokeza uwe nalo makini sana nisuala la ajira zinazotolewa na TAMISEMI. Mfano hizo ajira 32 elfu zitakazotangazwa karibuni wahuni ndani ya wizara yako wapo kibao. Ajira zinatolewa lakini bado maswali mengi sana yako maana wapo watu waliokaa sana mtaani bila ajira na waliomaliza vyuo karibuni wanapata tena wenye vigezo vilevile. Mh Bashungwa simamia usawa na uwazi wa utoaji wa ajira ndani ya ofisi yako.
MAPENDEKEZO KUHUSU AJIRA.
Ili kuondoa sintofahamu kubwa iliyopo toeni ajira mkizingatia UMRI,MUDA WA KUMALIZA CHUO na sio kuchaguatu shaghalabaghala
Hongera kwa kazi nzuri Mh. Bashungwa endelea kufukiza moshi wahuni waliopo ndani ya ofisi yako ukianzia hapo wizarani makao makuu