Mh! Hii ya waswana haijatulia kabisa..!!

Mh! Hii ya waswana haijatulia kabisa..!!

Sajenti

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Posts
3,651
Reaction score
413
Leo asubuhi nilikuwa nikisikiliza BBC na katika moja ya taarifa zilizonishangaza ni kuwa nchini botswana kuna sheria inayomkataza mume au mke kumfatilia mwenza wake pindi mmoja wao anapoamua kutoka na mwanamke au mwanaume mwingine. Kwamba kama mwanaume atamkuta mkewe yuko bar au klabu anajivinjari na njemba mwingine ni kosa kwa mume kumfata huyo mke na kuhoji kinachoendelea pale hali hii pia ni kwa wanawake. mama akimkuta mzee yuko bar na sholi mwingine haruhusiwi kabisa kuwaghasi. Na katazo hili linakuwa pale inapotokea kama mume au mke huyo hawakutoka pamoja kwenda mahali pale. Pia ni kosa mume au mke anapokuwa amesafiri kikazi nje ya nyumbani kwake zaidi ya wiki 3 kurudi nyumbani kwake bila ya kutoa taarifa kwa mume au mke kwa simu kuwa unarudi nyumbani kutoka hiyo safari yako ya kikazi....Sasa kali zaidi ni kuwa inapotokea mume au mke amerudi kutoka safari ya kikazi bila kutoa taarifa utakachokuta nyumbani kwako unatakiwa kuwa kimya. Kwa maana kuwa kama mzee ndio unarudi kutoka safari kimya kimya ukikuta mama ameingiza njemba nyingine nyumbani kwako wewe unatakiwa kuwaheshimu na kutowafanyia fujo........Hii ingekuwa hapa bongo nina imani watu wangekatana shingo mchana kweupe hata kama ndio sheria.....:twitch::twitch::A S-eek::A S-eek:
 
Labda ndo maana wanakaribia kwisha kwa ngoma...
 
mmmh!!!!!!!! duniani kuna mambo.... sasa hata huko botz wanazigatia kweli?.... nina wasiwasi kama hii sheria inafanya kazi sawasawa....
 
Hii kitu ilikuwepo katika mila zetu....ilikua mzee akitoka, anaporudi huwa haendi nyumbani moja kwa moja. Ilikua anapokaribia hutanguliza chochote kinachotambulisha kwamba karudi, iwe ni furushi au hata koti! Kwa hiyo B'swana wanadumisha tu mila hapo....:A S 39:
 
Hii kitu ilikuwepo katika mila zetu....ilikua mzee akitoka, anaporudi huwa haendi nyumbani moja kwa moja. Ilikua anapokaribia hutanguliza chochote kinachotambulisha kwamba karudi, iwe ni furushi au hata koti! Kwa hiyo B'swana wanadumisha tu mila hapo....:A S 39:
He! nimekushangaa sna kusupport hii kitu duh!
 
.....Botswana bila ukimwi itawezekana kweli?
 
He! nimekushangaa sna kusupport hii kitu duh!
..Salha, kila kitu kina uzuri na ubaya wake. Niliwahi kwenda wilaya ya simanjiro mkoani manyara kikazi. nilipata nafasi ya kuongea na wazee, vijana na akina mama wa kimasai. Kule hakuna kesi za watu kugombania wanawake. Ni kwamba mwanamke wa kimasai ni wa kila mwanaume wa kimasai kulingana na rika alimo huyo mume. Na wao wanakwenda mbali zaidi ikitokea mwanaume mzamiaji amemtia mimba mwanamke mtoto atakayezaliwa atakuwa ni mtoto wa mwenye mke.....We si umesikia huku uswahilini kwetu kila siku story za watu kufumaniana, kupigwa, wengine mpaka aliyefumaniwa analawitiwa eti kumkomesha...Tatizo hapa je maradhi yatawakosa hawa watu??
 
Mkuu Sajentu hata mi nimeisikia hii stori asubuhi sema kwa vile nilikuwa kwenye mambo ya 'kwa msaaada wa watu wa marekani' sikuisikiliza kwa makini,,,, niliikuta mwishoni mwishoni

lakini ni kity kilichokuwepo hata kwetu kama alivosema Roya Roy apo juu

unarudi unapiga kamluzi kutoa ishara kwamba mwenye boma ameingia...hii ilikuwa inapunguza sana misuguano

Uzuri enzi hizo kulikuwa hakuna magonjwa ya ajabu ajabu kama UKIMWI nk.......

sasa hivi haya ya kuvunja ukimya sijui ndo tunaelekea huko ama vipi? Hivi huu wivu wa siku hizi inakuwaje au ni 'socially constructed'? Manake hao mababu zetu na hao watswana sasa hivi, kwao hakuna wivu na ubinafsi tulio na wengi wetu?
 
Mnakwepa swali la msingi........................mko tayari itumike kwenu?:shock:
 
Kwa karne hii ya AIDS ni sheria nzuri sana kuwanayo hapa TANZANIA ili wote tufe kwa ngoma. Hii nimeipenda kwani imetulia
 
Na ukimwi unavyowachapa mijeledi basi....!!!
 
Na ukimwi unavyowachapa mijeledi basi....!!!

Mkuu sidhani kama hiyo ndio sababu kuu ya hawa jamaa kuwa na rank ya juu kwa maambukizi.... Mbona Tz nayo iko juu vile vile?
 
Back
Top Bottom