Mh. Lowassa, Sumaye hawawezi kubaki upinzani milele.

Mh. Lowassa, Sumaye hawawezi kubaki upinzani milele.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Hawa ni watu ambao walitaka kuipitia njia "ndefu" ya mchepuko ya upinzani chapuchapu ili kuwafikisha kwenye njia kuu ya kuingia Ikulu lakini sio watu wa kuishi na kudumu kukaa na kuishi maisha ya upinzani yenye shida, tabu na mashaka mengi.

Baada ya njia hii kushindikana kuwafikisha Ikulu mwaka 2015 watu wote hawa pamoja na wale waliokuwa wanataka kumsindikiza Mh. Lowassa na kundi lake kwa kupitia uchochoro huu wa upinzani kuwafikisha Ikulu lazima wote "watatubu" na kurejea kwenye chama chao walichoshiriki kukianzisha, kukilea, kukitumikia na wanachokifahamu vizuri. Na hata angekuwa mimi au wewe ungefanya hivyohivyo wasilaumiwe kama watarudi walikotoka, kwakuwa hawa waheshimiwa wana mali njingi sana, siri nyingi sana na maslahi mengi sana ambayo hayawezi kulindwa vizuri kama wataendelea kubaki upinzani kwa muda mrefu. Kutokana na muundo wa nchi yetu na CCM ilivyo, wengi wa watu hawa ni usalama wa nchi tosha.

Kama uchochoro huu ungefanikisha kuwakutanisha na barabara kuu ya kuelekea Ikulu basi akina Mbowe na wenzake nao wangefanikiwa kuambulia harufu kidogo ya keki, lakini kwakuwa haikuwezekana basi akina Mbowe msilalamike wala kushangaa sana kumuona Mzee Kingunge akisema "CCM ni chama changu siwezi kwenda kinyume na matakwa yake" mbele ya mwenyekiti wa CCM pale kitandani Muhimbili. Kosa kubwa na dhambi kubwa mliyoitenda akina Mbowe ni kuwasukuma Dr. Slaa na Prof. Lipumba bila heshima wala maelewano wakati mnampokea Mh. Lowassa. Dhambi hii itawatafuna hadi mifupa yenu.

Hata hivyo chadema na UKawa MNA BAHATI KUBWA SANA KWAkuwa haya yote yanatokea leo miaka 3 kabla ya uchaguzi, angalau mna muda wa miaka 2 au 3 ya kutafakari kwa kina kuhusu 2020. Wanachama na mashabiki wetu bado mnao mpaka sasa lakini Kazi yenu kubwa mbele yenu ni kutafuta vyanzo vya mapato sasa hivi na leoleo ya kuendeshea uchaguzi mwaka 2020.

Ushauri wangu wa bure kwenu acheni kumjadili Mh. Lowassa na Kingunge kwa kile walichokifanya na kukisema ili kuibakiza heshima yenu mbele ya mashabiki zenu. Mh. Lowassa anafahamu vema kile alichokifanya lakini ninyi hamkifahamu vema kile alichokikusudia kwa kufanya vile.

Mnajua ni kwanini Mh. Lowassa hakutukana hata kidogo ingawa yeye alitukanwa, kubezwa, kutaniwa, kukejeliwa?
 
Back
Top Bottom