Mh.Pinda akiri: Kuna tatizo Serikalini

Mh.Pinda akiri: Kuna tatizo Serikalini

Ibrah

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2007
Posts
2,730
Reaction score
530
Kuna tatizo serikalini-Pinda

Habari Zinazoshabihiana
• Spika apiga marufuku mjadala wa Pinda 15.07.2008 [Soma]
• Pinda ashikilia kauli yake kuhusu Zanzibar 11.07.2008 [Soma]
• Pinda: Hatuogopi mafisadi wa Richmond, EPA 08.07.2008 [Soma]

*Acharukia ma-RC, ma-DC, wakurugenzi
*Asema migomo, maandamano ni kawaida

Na Mwandishi Wetu

BAADHI ya watendaji wakuu wa Serikali mikoani hadi wilayani ni dhaifu na ndicho chanzo cha matatizo yanayoikabili Serikali hivi sasa, imeelezwa.

Hayo yalisemwa jana na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, alipokuwa alizungumza na wahariri wa vyombo vya habari ofisini kwake Dar es Salaam.

Alisema usimamizi mbovu wa viongozi hao ndio umesababisha wananchi wasitatuliwe matatizo yao kwa wakati na hivyo kuleta migomo isiyokuwa na maana.

"Baadhi ya wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri zetu, wapo kusubiri mishahara tu, hawatusaidii kabisa," alisema Waziri Mkuu na kuwataka waondoke ofisini na kwenda kusaidia wananchi vijijini.

Bw. Pinda alisema kutokana na udhaifu huo, ndiyo maana kumekuwa na urasimu mkubwa katika kutatua matatizo ya wananchi, wakiwamo walimu na kusababisha wagome wakati ambao hawakutakiwa kufanya hivyo.

Akifafanua kuhusu mgomo wa walimu, alisema utaratibu uliopo katika kushughulikia walimu wapya ni mrefu na hasa pale wakurugenzi wa halmashauri wanapopokea fomu za walimu hao na kukaa nazo mpaka ziwe nyingi ndipo wazishughulikie.

"Hili kwa kweli limechangia katika matatizo haya, tunachokitaka ni Mkurugenzi akipokea fomu moja aipeleke kunakohusika, badala ya kukaa nazo mpaka eti ziwe nyingi.

"Urasimu ndilo tatizo, tunajaribu kulikabili kwa kutumia wakurugenzi hao hao ili lisijirudie...pia tutafuata ushauri wa Rais wa kuingia katika kutumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano, badala ya kuendelea kubeba majalada haya ya kizamani, ili tuharakishe kuhudumia wananchi," alisema.

Kuhusu malalamiko kuwa fedha zinazolipwa hazilingani na walimu walizokuwa wakidai, alisema ndiyo maana ya kufanyika uhakiki, na kwamba kila mwalimu aliyelipwa baadaye atapewa maelezo ya jinsi malipo hayo yalivyofikiwa, ili kuondoa malalamiko.

Akizungumzia mgomo wa wanafunzi wa elimu ya juu nchini, Waziri Mkuu alisema kamwe Serikali haitakopesha wanafunzi wote kwa asilimia 100 kama wanavyotaka, kwa sababu kuna baadhi ya wazazi wenye uwezo wa kulipia watoto wao hata kama ni kwa kuchangia kiasi fulani.

Alisistiza kuwa dawa ya mgogoro wowote ni watu kukaa chini na kuzungumza badala ya kutumia ubishi na nguvu na kusisitiza Kamati ya Pamoja ya Uongozi wa Vyuo Vikuu nchini (TAHLISO) na Serikali kuendelea kukutana na kujadili matatizo yaliyopo.

Alivitaka pia vyombo vya Serikali kuwa makini katika kushughulikia matatizo ya umma, ili jamii isifikie kwenye migomo.

Kuhusu mgogoro wa wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Waziri Mkuu Pinda, alisema pamoja na hatua kuchukuliwa kwa mazungumzo, bado kuna fukuto la malalamiko na hivyo Serikali sasa imeamua kumshughulikia mstaafu mmoja mmoja badala ya kundi.

"Tumeamua kushughulikia mmoja mmoja ili tuchambue na kuwatendea haki, kwani kama kundi tunashindwa kujua yupi anadai kipi na ashughulikiwe vipi," alisema.

Kuhusu kilimo, Waziri Mkuu alisema bado wasimamizi wa sekta hii hawajakidhi mahitaji kutokana na kutoelewa ni nini wajibu wao kwa wakulima na ndiyo sababu wanakaa ofisini bila kuwafikia wakulima na hawatumiki ipasavyo.

Alisema ili kuleta tija katika kilimo, Serikali inafikiria kuanzisha mashindano ya uzalishaji kuanzia ngazi ya mkoa hadi mtu mmoja mmoja, ambapo Siku ya Wakulima ya Nane Nane mwakani, ndiyo itakayoonesha utekelezaji wake.

Akizungumzia elimu, alisema bado kuna changamoto mbalimbali katika upungufu wa walimu hususan wa masomo ya Sayansi na kupongeza juhuydi za uanzishaji wa shule za awali katika shule nyingi za msingi nchini na ujenzi wa sekondari za kata.

Kuhusu sakata la EPA hususan malalamiko ya baadhi ya watu ya kutaka wamiliki wa kampuni ya Kagoda Agricultural Limited wafikishwe mahakamani, Waziri Mkuu alitaka Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) aaminiwe.

"Kama wengine wamefikishwa mahakamani na DPP huyu huyu, kuhusu Kagoda ataamua tu, kwani kutokana na mashinikizo haya yaliyopo, kila jambo litaanikwa tu ," alisema Waziri Mkuu.

Akizungumzia kuliimarisha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), alisema ni kipaumbele chake na Serikali inahangaika kwa nguvu zake zote kuhakikisha kuwa ATCL inarudia kutoa huduma vizuri zaidi.

Alisema inakabiliwa na matatizo mengi yakiwamo ya upungufu wa ndege, marubani na madeni mbalimbali ya mafuta na kadhalika.

Kuhusu madai kuwa Serikali imelemewa, Bw. Pinda alisema hilo halipo na migogoro inayoendelea ni ya kawaida na ni changamoto ya Serikali kupambana nazo.

"Haya yalikuwapo hata katika miaka mitano ya kwanza ya Rais Ali Hassan Mwinyi, mnakumbuka mihadhara mbalimbali na nini...miaka mitano ya awali ya Rais Benjamin Mkapa, pia kulikuwa na matatizo na hii ya Mzee Kikwete nayo ni hivyo, lakini katika miaka mitano ya pili mambo yatakuwa shwari," alisema.

Akijibu swali kuhusu hatima ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dkt. Edward Hosea na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Johnson Mwanyika, kuhusu sakata la Richmond, Waziri Mkuu alisema itajulikana tu.

Alisisitiza kuwa viongozi hawa nao wana haki ya kusikilizwa, hivyo lazima wasikilizwe ndipo hatua zichukuliwe. "Kuna mambo makubwa ya kufanyiwa kazi ma kutolea uamuzi si kama tunavyoliona."

Akizungumzia kampuni ya reli ya TRL, alisema madai kuwa 'anaibeba' si sahihi na kwamba anaisaidia kwa kuwa ni chombo muhimu na nafuu cha usafiri wa wananchi wa kawaida hasa wa mikoani, lakini Serikali ina hisa nyingi, hivyo haiwezi kuikwepa.

Akijibu madai kuwa Serikali ina matumizi makubwa ya magari ya kifahari, alikubali na kueleza kuwa anachoangalia yeye si gharama ya magari, ila ni kama magari hayo yanazalisha tija, kinyume chake hayana maana.

Kuhusu kufungiwa kwa gazeti la MwanaHalisi huku Habari Leo likiachwa, Waziri Mkuu alisema Serikali ilichukua hatua baada ya kujiridhisha kuwa kilichofanyika na maelezo ya Mhariri wake hayakuwa yanatosheleza.

Aliongeza kuwa Habari Leo, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, analifanyia kazi na hatua zitajulikana kama alivyoahidi bungeni katika Mkutano uliopita Dodoma.

MwanaHalisi ilifungiwa baada ya kuwataja kwa majina wenyeviti wa CCM wa mikoa minane nchini kwamba wamepanga kumng'oa Rais Kikwete katika kinyang'anyiro cha urais mwaka 2010 huku wakimhusisha mtoto wa Rais, Bw. Ridhwan Kikwete.

Habari Leo katika habari inayolalamikiwa, iliandika kuwa baadhi ya wabunge (bila kuwataja) walipanga njama za kupinga msimamo wa Rais Kikwete kuhusu mapambano dhidi ya wezi wa fedha za EPA.

Waziri Mkuu Pinda hata hivyo, alisisitiza wanahabari kuzingatia maadili ya taaluma yao ili kuepuka matatizo na migogoro kama hiyo hata kufungiwa.

Source: Majira 25 Nov

Katika kipindi cha pwer break Fast cha cloud FM leo, nilimsikia Uncle G akimsifia Waziri Mkuu Pinda kuwa yeye si kama wanasiasa wengine wa TZ walivyo na ya kuwa huwa hachanganyi issues za Kiserikali na Kisiasa, anapozungumzia siasa anafanya siasa na anapozungumzia serikali anazungumzia utendaji.

Sina hakika na kauli za Gerald Hando lakini ukweli ninampenda Pinda tangu akiwa Naibu Waziri TAMISEMI. Nilimpenda Pinda kwa utendaji wake na kuwa mkweli hata pale mambo yanapoenda kombo. Nilimpeda zaidi wakati akijibu maswali kama Naibu Waziri wakati ule (Brg Ngwilizi akiwa Waziri) na kwa hakika Brg Ngwilizi alifunikwa kabisa na Pinda na ni kama vile Ngwilizi alimwachia kila kitu Pinda na ukweli ni kuwa ali-fit vizuri na haikuwa ajabu alipoingia JK akamteua kuwa Waziri kamili TAMISEMI kabla ya kumpa Uwaziri Mkuu. Alipoteuliwa kuwa waziri mkuu nilitegemea kabisa kuwa anastahili lakini baada ya muda nikaanza kumuonea huruma kuwa nafasi waliyompa ya Uwaziri Mkuu ilikuwa ni kumuonea. Hii ni kwa sababu Waziri Wakuu waliomtangulia walikuwa Wanasiasa zaidi kuliko kuwa Watendaji na kwa kuwa Pinda si mwanasiasa sana (kwa maaana ya porojo) angepata wakati mgumu kufanya kazi yake na hii naithibitisha kwa kauli yake Bungeni wakati akijibu swali la moja kwa moja kuhusu MEREMETA alipposema kuwa MEREMETA Co ni suala nyeti kwa Usalama wa Nchi!

Gazeti la Majira limemnukuu Pinda akikiri kuwa kuna Tatizo Serikalini kitu ambacho Watangulizi wake (Sumaye na Lowasa) wasingekubali. Namuone huruma Pinda kwa kauli zake za ukweli ambazo mara nyingi penye udhaifu amekiri udhaifu kitu ambacho ni hatari kwa Serikali anayoiongoza na Chama chake CCM ambacho nakiona kuwa hakijazoea kusema ukweli.

Lakini pia nafurahi kuwa Pinda amekiri kuwa kuna Tatizo Serikalini na ukweli ni kuwa mimi binafsi naona kuna tatizo kubwa upande wa viongozi wa mikoa Ma-RC na Ma-DC.

KWangu mimi naona kuwa viongozi hao ni wa Kisiasa zaidi ambao wanaongeza gharama bure za uendeshaji wa serikali maana china yao wapo Ma-DAS wa Wilaya na Mikoa na nadhani wakati umefika kuondoa hivyo vyeo vya Ma-DC na Ma-RC pengine tubaki na Makatibu Tawala tu wa Mikoa na Wilaya maana vyeo vya Ma-DC na Ma-RC vinatolewa kisiasa kwa Wanasiasa kwa Manufaa ya Kisiasa kwa gharama ya Wananchi na hivyo kuongeza gharama za uendeshaji wa Serikali. Mishahara na Magari wanayolipwa na kutumia ni mapesa mengi mno kwa nchi yetu changa na naamini kabisa kuwa tukiachana na watu hao, Serikali yetu itaongeza uwezo wake wa kufanya miradi na shughuli za Kimaendeleo.

Hebu tafiti Wakuu wa Wilaya na Mikoa uwajuao, tafiti elimu zao na Uwezo wa Utendaji wao ndipo utajua kuwa ni vyeo vya Kisiasa tu na wengi wengine wao ama ni marafiki wa Viongozi wakuu au ni Walikuwa wapiga debe wao wakati wa chaguzi na ni Makada wa CCM (Mfano Bibi Mwilima, DC wa Hai, kutoka Wenyekiti wa Tawi la CCM hadi U-DC!). Wengine wao ni Wabunge walioshindwa kwenye chaguzi mfano Moshi Mjini (Samizi), Mbeya (Mwakipesile na Quares) Tabora (Abeid Mwinyimsa), Tarime (Mabiti), Mbega (Ruvuma). Mwanza (Eng. Msekela bado ni Mbunge pia), Dodoma (Lukuvi bado ni Mbunge pia) wana Mashangingi ya Ubunge na Ukuu wa Mkoa. nk,nk. Mara nyingine vyeo hivyo vimetumika kama adhabu mfano Col. Simabakalia (kutoka MD-NDC hadi ukuu wa Mkoa Kigoma).

Nadhani wakati umefika wa kutafuta mfumo mwingine ambao hautakuwa na gharama ama kuachana kabissa na vyeo hivi. Inawezekana wakati wa Nyerere ilikuwa hatuna budi kuwa na vyeo hivi lakini kwa wakati wa sasa sioni umuhimu wa vyeo hivi.
 
Back
Top Bottom