Eddy, mimi sijasema yuko kimya kwa kufuata ushauri wa wazee, ila nimesema serikali ilitoa amri ya kusitishwa kwa malumbano mara moja baina ya RA na Mengi.
Mimi hoja yangu ni kwenye ufisadi, Watanzania wengi tuko nyuma ya yeyote yule anayepigania mustakabali mwema wa nchi yetu. Na sidhani kama bahasha ya RA ina cha maana ni danganya toto tu na kuwazuga Watanzania who cannot think outside the box. Kama RA angekuwa na la maana hakupaswa kusubiri hadi atuhumiwe ndio awasilishe hiyo bahasha yake. Kuhusu Hosea, chuo alichosemea hakitusaidii chochote, maana ufisadi ni suala la maadili na sio elimu, ingekuwa ni elimu Andrew Chenge kasomea Havard lakini yako wapi?