Makala Jr
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,395
- 1,112
Wasalamu ndugu; Mara nyingi huwa natenga muda kuchunguza yanayozungumzwa na viongozi leo kwa kulinganisha na yale waliyonena jana. Kama ilivyo ada kwamba mkubwa ni jalala, nimeamua kupima kauli za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa JMT Mhe.Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na kugundua kwamba pengine anasahau haraka kauli zake au anashindwa kuufanya umma uelewe ni wakati gani anazungumza kama Rais/Mwenyekiti wa CCM. Ni majuzi tu alinukuliwa na vyombo vya habari akisema, "Wana CCM wajiandae kisaikolojia endapo wananchi wataamua muungano wa serikali 3". Lakini kwenye sherehe za maadhimisho ya kuzaliwa CCM, amesema msimamo wa CCM ni serikali mbili na wanaotaka serikali 3 wawashawishi wana CCM.Hoja inaibuka hapa, Mhe.Warioba aliongoza tume yake kukusanya maoni ya nani kama si wananchi wenyewe? Ni vishawishi gani anavyovitaka Mhe.Kikwete na wana CCM wengine ili wakubaliane na tume ya Jaji Warioba? Na je, suala la katiba linahitaji maoni au misimamo?