MJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba, John Shibuda amesema msimamo wake ni kuwapo kwa Serikali mbili, huku akisisitiza kuwa ilipaswa wajumbe wa bunge hilo wapewe elimu ya ufahamu ya kazi yao.
Akizungumza katika viwanja vya Bunge jana, Shibuda ambaye ni Mbunge wa Maswa Magharibi kwa tiketi ya Chadema, alisema hata kama itamlazimu kufukuzwa katika chama, msimamo wake ni muundo wa Serikali mbili.
Msimamo wa Chadema katika muundo wa Serikali ni kuwapo kwa Serikali tatu, muundo ambao pia umependekezwa katika Rasimu ya mwisho ya Katiba, iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ambayo itawasilishwa katika Bunge hilo.
Wakati Chadema ikijinadi kwa mfumo huo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinataka kuwapo kwa mfumo wa Serikali mbili, na wajumbe wake ndani ya Bunge wataeleza kwa nini kinataka mfumo huo.
"Ndio nataka mfumo wa Serikali mbili. Wale Wasukuma wangu, wafugaji na wavuvi wangu nitawaeleza nini.Mimi nimetumwa na watu, na nitasimamia mfumo huo," alisema Shibuda.
Alisema kumekuwapo na uhusiano wa karibu kati ya watu wa Tanzania Bara na Zanzibar kwa miaka 50, wakiwamo Wasukuma, ambao alisema wapo Visiwani na Bara, na wamekuwa pamoja kwa miaka yote hiyo.
"Kuna makabila zaidi ya 130 hapa. Yana uhusiano wa moja kwa moja, wakiwamo Wasukuma ambao ni asilimia 30 ya Wazanzibari. Sasa hawa niseme siwataki," aliongeza Shibuda.
Aliwafananisha wanaokataa Serikali mbili sawa na mtoto anayemkataa babu yake, kwani ni sawa na kuikana historia yake.
"Kuna watu hawajui hata historia ya Tanzania. Hawajui historia ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar. Hawajui Tanganyika ilipataje uhuru. Hawajui Zanzibar ilivyopata Uhuru wake. Kuna sintofahamu kubwa," alisema Shibuda na kupendekeza kwanza wajumbe wangepitishwa kufahamu historia ya nchi.
Alisema uanaharakati na uprofesa ni vitu tofauti linapokuja suala la historia ya nchi, hivyo kwa sababu ya kuwa na wajumbe wa aina mbalimbali katika Bunge hilo, kulipaswa kuwa na uelimishwaji kabla.
"Hata kama Rasimu ya Kanuni itakuwa nzuri, haisaidii kitu. Kuna sintofahamu ya uelewa kwa wajumbe, hivyo hili lilipaswa kwanza tuelimishane," aliongeza mwanasiasa huyo machachari.
Bunge Maalumu la Katiba halijaanza mijadala yake likisubiri kukamilika kwa Kanuni ambazo kuanzia leo kwa siku mbili, wajumbe watajadili Rasimu ya Kanuni. Baada ya kuridhiwa kwa Kanuni hizo, ndipo utafuata uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti na baadaye viapo kwa wajumbe, kabla ya ufunguzi rasmi wa Bunge hilo lenye wajumbe 629.
Ufunguzi utafuatiwa na kuwasilishwa kwa Rasimu ya Katiba, na ndipo mjadala sasa utaanza wa kuichambua Rasimu hiyo, huku eneo la mfumo wa Serikali likitarajiwa kuwa na mjadala mkali. Katika hatua nyingine, wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba ambao ni wabunge wa CCM, walikuwa na kikao jana kuanzia saa moja usiku.
Inaelezwa kuwa kikao hicho kilikuwa mahsusi kwa ajili ya kuweka msimamo katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge, ambao makada wao wawili, Samuel Sitta na Andrew Chenge wanaaminika kukitaka kiti hicho.
Source: Habari Leo