Mh Temba: Fedha imeisambaratisha Yamoto Band

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598


Dar es Salaam. Mashabiki wengi wa muziki nchini bado wapo katika sintofahamu juu ya sababu ya kuvunjika kwa kundi la Yamoto Band, mwanamuziki Mh Temba ametoboa siri hiyo.

Tangu kusambaratika kwa kundi hilo mara kadhaa wanamuziki hao wamekuwa wakikanusha, lakini mwendo unaoendelea ni kuwa hali katika kundi hilo si shwari tena.

Katika moja ya mahojiano Mh Temba alisema kusambaratika kwa kundi hilo kumetokana na fedha kuingilia kati na hivyo kusababisha kila mmoja kutaka kuwa na sauti yake.

“Mimi nakupa mfano hawa Yamoto, utaona labda kuna mtu anasimamia msanii fulani, mbona hakumchukua mwanzo wakati hajulikani kabla hatujamkuza na kuwa superstar,” amesema Temba.

“Huyo mtu kama ana uwezo kwanini asingekuwa na vipaji vyake, wewe unaona tayari nuru inang’aa unaenda kuchomoa pale,” ameongeza.

Kundi la Yamoto liliundwa na Aslay, Maromboso, Beka Flavour na Enock Bella ambao kwa sasa kila mmoja anafanya kazi peke yake.


Mwananchi
 
It's always like that money n women (sorry kwa mama zetu)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…