Utafiti wako umeufanyia wapi?
Umeuliza wanawake wangapi ili kupata jibu la 95%
Hii ya kwenda kwa mganga nayo umeifanyiaje utafiti?
Una maana kati ya wanawake 100 walioko kwenye ndoa 85 wamekwisha onana na maji marefu ili kupata hirizi ya kupendwa?
Sas hili la 80% ya wanawake walioko kwenye ndoa kufujwa sijui unamaanisha nini?
Mimi niko kwenye ndoa miaka 21 bado sijui undani wa ndoa za watu kibao hadi wale ambao nimeshiriki kutatua matatizo yao ya ndani mpaka yakaisha.
Kuna kumchoka mtu kwa vitabia au kwa kudhanibucha ya pili nyama ni nzuri zaidi.
Binadmu yangu alisha wahikumwacha mama mtoto wake kisa ni mshamba haendani na wakati hii ni kama 16 years a go.
Basi mimi na mke wangu tukamfuata yule mama wakati huo akiwa binti kazaa mara 1 tu tukamhoji akatueleza mengi.
Mke wangu akaamua kufanya jambo moja ambalo mimi sikuwahi kufiriki.
Tulimtafuta fundi mzuri wa nguo za kike tukamshonea sketi 3 blauzi 3 na magauni 2
za ndani safi pafyumu na pea mbili za viatu
binti akatinga saluni wakamfumua twende kilioni zake na kumsuka vizuri.
Kisha tukamwambie ajipitishe mitaa ya Sinza anakoishi yule binamu yangu.
Rafiki zake walipomwona habari zikamfikia binamu yangu ikabidi afanye juu chini akutane na mama mtoto wake naye ajionee.
Siku walipo kutana jamaa taya la chini nusura lijipigize chini huku mimacho imemtoka.
Akamwangukia na hakumwona mshamba tena.
Asilimia 95 ya wanawake walioko kwenye ndoa na mahusiano hawafiki kilele wakati wa tendo la ndoa,lakini robo tatu ya asilimia hiyo hawajui kama mwanamke naye hufika kilele!Wakati huohuo asilimia 85 ya wanawake walioko kwenye ndoa ama wameshaenda kwa mganga kupewa dawa za kuwafanya waume zao wawapende au wanatafuta waganga hao ili kupata dawa.Lakini asilimia 80 ya wanawake walioko kwenye ndoa/uhusiano wanafujwa(abuse)kwenye ndoa au uhusiano.Lakini ni asilimia 98 ya wanawake wote hawako tayari kuishi bila waume.Na asilimia 6 ya wanawake walioko kwenye ndoa hufa kila mwaka kutokana na matatizo ya kindoa!. . . . . .Wanawake mna matatizo gani?