MH. Waziri mkuu, tafadhali, chonde msiwachefue walim na Tume ya uchunguzi matokeo 4m4

mansakankanmusa

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Posts
4,162
Reaction score
796
Tume
itakayo mhoji mwalimu eti kwa sbb wanafunz wamefeli itakuwa imekosea
kabisa,

Wakuu wa shule weng nchn ni maadui kwa walimu wao, maana wanamtumikia
bwana

Serikali ni ya mungu binadamu ni watendaji tu, ni kawaida binadamu
kukosea lakini si kukosea kabisa. waziri mkuu usipotoshwe. ukitaka
majibu ya tume hyo waweke walimu wakawaida sio timu yako hyo. pia walimu
wamenyimwa haki nying je unataka majibu yapi kwao?
Sitashauri kuwafwata walimu, ni busara muwalipe pesa zao, mh. Rais atumie mamlaka yake kuwapendekezea mshahara mkubwa, elimu ni roho ya nchi nying duniani. Kabla ya kuwadai wajibu wao wapeni haki yao.
Wanalipa nauli nao kwenda na kurudi shuleni,vituoni mwao, kila siku. Wanalipa kodi zao kila mwezi, kwa mshahara upi?
 
Napendekeza,kila mwalimu wa somo fulani sekondari afanyishwe mtihani wa kipindi anachofundisha,kwa paper ile ile ya 2012,itaisaidia tume kujua exactly tatizo liko wapi,nina uhakika hata hao waalimu wanaodai eti wamegoma na ndio sababu matokeo yamekuwa mabaya ,wengi wao wakifanya paper hizo watapata matokeo yale yale ya wanafunzi wao,wengi wao uwezo pia ni mdogo ila tu wanataka kutumia mwanya wa matokeo mabaya ili kupata nyongeza za mishahara,hakuna cha mgomo wala nini,uwezo wao umeishia hapo.Shule nyingi za private na seminary ambazo matokeo ni mazuri wana tabia ya kutafuta waalimu wanao faulisha vipindi fulani,wanashawishiwa kwa mishara mizuri na kuhamia shule zao,wengi wanaobaki shule za kata wana uwezo mdogo,hata ikitokea akawepo mwenye uwezo kama ikitokea somo lake wanafunzi wakafaulu utasikia baada ya miezi kahamia FEZA etc
 

Na wewe hapo umeandika au umeharisha?
 

sawa great sinker
 
Hii inaitwa witch-hunting
 
sababu za kufeli zipo wazi, ni kipi ambacho serikali haikifahamu juu ya kufeli kwa wanafunzi hawa? kwa mtazamo wangu wanafunzi wenyewe ni sababu tosha kwani hawaoni umuhimu wa kusoma anasa nyingi, na pia sioni haja ya yeyote kuwajibika zaidi ya wazazi wakifuatiliwa na wanafunzi wenyewe kubadilika, wanafunzi hawajaanza kufeli mwaka huu bali kila mwaka kiwango cha kufeli kinaongezeka sasa kama mwanafunzi anaingia fom 1 hajui kusoma wala kuandika unategemea afaulu? atasubiri afauulishwe tena kuingia kidato cha tano bila juhudi zake. Cha msingi naisihi serikali iiangalie upya sekta ya elimu. utendaji umekuwa mbovu kuanzia katibu mkuu na wasaidiz wake hadi mwl wa chekechea
 
Kuhusu kila mwl kufanya iyo pepa nakubali ila je wasahishaji nao watapimwaje? maana km pia una2mia marking scheme vp hpo
 
Hii tume itakuwa na kazi ngumu kwa sababu naona kila mtu atajitetea:
Wanafunzi watajitetea hivi
  1. Hakuna walimu wa kutosha
  2. Hakuna maabara na maktaba
  3. Upungufu wa vitabu
  4. Hakuna madawati pia madarasa machache tunabanana kwenye darasa moja wanafunzi 80-100
  5. Tunasafiri umbali mrefu hivyo tunachoka sana
  6. Hatupewi chakula shule
  7. Walimu hawakai shule muda mrefu,mwalimu anafundisha mwaka mmoja anaondoka
  8. Tunafanya kazi nyingi nyumbani badala ya kujisomea

Mwalimu naye huenda akajitetea
  1. Mishahara midogo
  2. Hakuna posho ya kufundishia
  3. Hakuna vitendea kazi
  4. Tunakaa mbali na mazingira ya shule
  5. Tunarundikiwa vipindi vingi vya masomo
  6. Hatupewi semina pindi topic mpya zinapoongezwa
  7. Wakuu wa shule pamoja na maafisa elimu wanatunyanyasa
  8. Gharama za Maisha kupanda hivyo lazima kufanya shughuli nyingine ya kuongeza kipato
  9. Wazazi hawatupi ushirikiano katika malezi ya watoto
  10. Wanasiasa kuingilia mipango ya shule:mfano baadhi ya wanafunzi ambao hawakufalu darasa la saba wanaingia sekondari kwa shinikizo la wanasiasa wengi wao wakiwa ni madiwani wanaoziita shule za kata ni zao

Ni hayo tu ongeza mengine
 
visingizio tu. waalimu wanatakiwa kulipwa kiasi gani ili wafanye kazi kwa bidii? mbona ni Serikali nzima matatizo ni hayo hayo?
 
visingizio tu. waalimu wanatakiwa kulipwa kiasi gani ili wafanye kazi kwa bidii? mbona ni Serikali nzima matatizo ni hayo hayo?

Tatizo la walimu sio mishahara kiuhalisia ila tatizo ni kuwa hawana posho yoyote ukilinganisha na kada nyingine,kwa mfano akipata laki tatu basi hakuna hela nyingine anayotegemea kupata mpaka mwisho wa mwezi
 
Natumain ukwel unajulkana chanzo ni mfum/serikal, wazaz, wanafunz, mazingira, siasa ktk elimu na walm wachache ambao hawaju nini maana ya haiba ya ualim/code of conduct/ethcs. mfn mwal kutembea kmwl na dent wake
 
hakuna jipya katika hiyo tume,serikali inajua tatizo. Na wataunda sana tume ila cha msingi waboreshe maisha ya walimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…