perfect.im24
New Member
- Aug 31, 2014
- 3
- 1

Mhe akisalimia na wanachama wa taasisi
Mbunge wa kigoma kaskazini Mhe. Zitto Zuberi Kabwe amefanikiwa kuzindua taasisi ya ENHANCE MASS DEVELOPMENT kwa kishindo kikubwa, ambapo uzinduzi huo ulifanyika tarehe 29/08/2014 katika ukumbi wa ABIOLA uliopo manispaa ya Temeke ambapo ulihudhuriwa na wanachama na wadau mbalimbali wapatao zaidi ya 700 wa taasisi hiyo.
Awali akisoma risala mkurugenzi wa taasisi hiyo ndugu Issa Mohamed alisema kuwa EMD katika kipindi cha mwaka mmoja tangu ilipo anzishwa emefanikiwa kupata wanachama zaidi ya 1003 ambapo wanawake ni 883 sawa na 88.04% na wanaume 120 sawa na 11.96%
Kwa kipindi cha mwaka mmoja jumla ya mikopo yenye thamani ya T,sh; 240,700,000/= imetolewa kwa wanachama wapatao 536.
Akisoma risala Mkurugenzi wa EMD alisema kuwa wanachama wanakabiliwa sana na changamoto ya uhaba wa mitaji na wakikimbilia benki inakuwa ni ngumu sana kwao kupata mikopo kutokana na riba kubwa inayotozwa na benki hizo pia ukosefu wa dhamana za kueleweka.
Akijibu risala hiyo MH; zito kabwe alisema kuwa njia rahisi ya kukabiliana na changamoto hiyo ni kwa wanachama kwa ujumla wao kwa kushirikiana na uongozi wa taasisi ya EMD kuanza mchakato wa kujiunga na mifuko ya kijamii hususani NSSF kwani watapata faida kubwa ya mikopo ya masharti nafuu na pia kupata bima ya afya kwa ajili ya maendeleo ya familia zao.
Pia alitoa shukrani za dhati kwa EMD kumpa mwaliko wa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo na kuahidi kuwa atakuwa bega kwa bega na EMD kuhakikisha malengo ya taasisi hiyo yanafanikiwa, katika kudhihirisha hilo ameamua kuanzia sasa yeye atakua mlezi wa taasisi hiyo, pia amewaasa wanachama kuwa linapokuja swala la maendeleo ni vema tukaweka itikadi za kisiasa pembeni na wote kwa umoja wetu tukaungana kuchangamkia fursa za maendeleo.
Mhe Zitto Kabwe akiingia ukumbini siku ya uzinduzi wa taasisi
MH; Zitto alipongeza pia taasisi hii kwa kuanzisha mchakato wa kutoa viwanja kwa wanachama kwa kusema kuwa hakuna rasilimali iliyo bora kama ardhi, kila mwana jamii anapaswa awe na sehemu ya kuishi ili apate utulivu. Jumla ya wanachama 95 wameshanufaika na mradi huo kati yao vijana ni 26 ambao wapo katika mradi pacha wa viwanja uitwao YOUTH VILLAGE
Kwa kudhihirisha kuwa amedhamiria katika kusaidia wananchi Mh; Zitto ameuagiza uongozi wa taasisi hiyo kuandaa mkutano mwingine kama huu ndani ya kipindi cha wiki mbili ili aje kuongoza harambee ya kutunisha mfuko wa asasi hiyo na pia kuwaomba NSSF waje kutoa elimu ya umuhimu wa wanachama wa EMD kujiunga na NSSF.
Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya EMD Bw; Issa Mohamed
Mwisho Mhe. Zitto alisema hakuna haja ya kulalamika lalamika kikubwa ni hiki mlicho kifanya cha kuungana pamoja nasisi kama viongozi kazi yetu kubwa ni kuongeza nguvu ili mafanikio yapatikane.
Tanzania Classic ikiongea na Mkurugenzi wa EMD Bwana Issa Mohamed kuhusiana na Mhe; Zitto kuwa mlezi wa EMD alisema haoni tatizo kwa muheshimiwa Z.itto kuwa Mlezi kwani amekuwa ni mmoja kati ya viongozi wanaojali zaidi maslahi ya umma na pia amedhihirisha kuwa ni mzalendo wa kweli, yeye pamoja na wanachama wa EMD wamefarijika na wanafuraha kubwa sana kwa Mh; Zitto kuwa mlezi wao na wanaamini kuwa ni mwanzo mzuri wa kusukuma mbele gurudumu la maendeleo

Mhe Zitto akiteta jambo na wanachama wa taasisi hiyo
