Mhadhiri Kibarua chaota Nyasi kwa kuhusishwa na siasa!

Mhadhiri Kibarua chaota Nyasi kwa kuhusishwa na siasa!

Mwalimu Mkuu

Member
Joined
Dec 26, 2010
Posts
62
Reaction score
39
aliyekuwa mhadhiri katika chuo kikuu cha Arusha mpiganaji Dadi Igogo amefukuzwa kazi katika chuo kikuu cha arusha kwa kuhusishwa na siasa chuoni hapo. 
 
pole sana dad, mungu ataendelea kukulinda, kazi nyingine utapata. ni fikra za kitumwa tu zinazowasukuma watu kufanya mambo kama ulilofanyiwa.
 
Yaleyale ya Mwesigwa Baregu! Komaa nao Dadi Igogo kuwaondoa hao wanamagamba inawezekana!
 
Kwanini achanganye mambo matatu matatu? ndio hawa wanahamasisha wadogo zetu migomo kila kukicha
 
Fundi halali njaa, Dad ni msomi na ninaamini atapata kazi nyingine sehemu ambayo wanaruhusu siasa, Keep fighting dad
 
We fisi kweli mhadhiri na mkopo wa mwanachuo una uhusiano gani? Mwanachuo akilala njaa kwakutopewa mkopo alioomba na kudhamini mali zake ama za nduguze atakuwa kahamasishwa na mhadhiri?

Wajinga kama wewe wasubiri kiama
 
huyu jamaa siasa iko kwenye damu na ni mpiganaji kweli tangu FASS na boom la wanafunzi mpaka AIA,!wana AIA wamempoteza mtu makini sanaa, usijali chief future still bright, swala la muda tu!
 
aliyekuwa mhadhiri katika chuo kikuu cha Arusha mpiganaji Dadi Igogo amefukuzwa kazi katika chuo kikuu cha arusha kwa kuhusishwa na siasa chuoni hapo. 

Angekuwa anapiga siasa za Magamba aaah angepewa hata ukuu wa chuo
 
Ujinga tu unatusumbua, angekuwa anafanya siasa za magamba wangepewa hata u VC kama mkandara!

Ujinga huu unaelekea mwisho wala hatukombali na mwisho wake.

Mtu mwenye elimu yake ambayo wewe ndo unaihitaji unapomfukuza kazi kwa misingi ya ubaguzi ni nani katika jamii anayekuwelewa?

Wanazidi kuongeza chuki ya wananchi dhidi ya serikali ya magamba. They will reap what they saw!

Pole mpiganaji lakini nadhani ulilitegemea hili na ulikuwa tayari kisaikolojia.

Hivi chuo cha uongozi cha CDM kinaanza lini ili hawa profs na phds walioko CDM watumike?
 
Huo Kikuu cha Arusha kinamilikiwa na Kanisa la Wasabato, hivyo ni chuo chenye mlengo wa kidini ya Kikristo. Kitendo cha Mhadhiri wa chuo hicho kujiingiza katika siasa ni kinyume na Dhima (Mission) ya chuo, hivyo kufukuzwa kwake kusidhaniwe ni kwa misingi ya makundi ya kisiasa mfano CHADEMA vs CCM n.k.
 
Dady ana msimamo, kwa Elimu yake anaweza kufanya kazi popote pale.Hata hivyo nadhani alishajiandaa kwa sababu alishaambiwa tangu Machi kama sikosei kwamba kibarua chake kipo matatani. Lakini nina mashaka na hizi Taasisi zetu. Ukiwa Mwana CCM unapewa hata Ukuu wa Taasisi. Tataizo ni Chadema
 
Dadi is an intellectual person, kwa sifa hiyo anaweza kufanya kazi popote. lakini naweza kusema hawa wote wanaoonewa na serikali ya magamba wakiamua kuanzisha chuo chao wanaweza kabisa, despite the fact that it may take a time to complete it.
 
Kwanini wasifukuze wabunge wa Upinzani Bungeni!?
 
Dadi Igogo,

wewe bado ni kijana. msomi na mtu thabiti...

mara nyingi ukiwa mtu jasiri na asiyeogopa, mwenye kujiamini, suala la mkate halitakusumbua..

hapa kuna mawili,KUhamia moja kwa moja uwanja wa mapambano usaidie kupeleka mbele jahazi la cdm na taifa kwa ujumla....

wakati huo huo kazi ni nyingi sana, PRIVATE SECTOR hata za kujiajiri pia sio lazima kufundisha....

utashangaa kwanini ulipoteza muda wako huko kwenye chuo cha wasabato...utajagundua kuwa Mungu huwa ana mpango na watu wake..ila there is function of tyme....to wait becomes inevitable

tuko wengi...tunasubiri pia barua zetu tuhamie kikosini full tyme!!!

USIOGOPE!
 
Back
Top Bottom