Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Msomi na Mhadhiri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mathew Mndeme, amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Mndeme amesema kuwa ameamua kuwania ubunge kutokana na kuona kwamba Jimbo la Arumeru Mashariki lina fursa nyingi za kiuchumi ambazo zingeweza kuwainua wananchi, lakini hazijatumika ipasavyo kwa sababu ya changamoto ya uongozi.
Aidha, ameeleza kuwa uzoefu wake wa muda mrefu katika uongozi na utatuzi wa changamoto mbalimbali umechochea uamuzi wake wa kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho, akiamini kuwa ana mchango mkubwa wa kuutoa kwa wananchi wa jimbo hilo.