Pre GE2025Mhamasishaji Michael Msechu na DC Petro Magoti wakutana kufanya ziara ili kuhamasisha vijana kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura
Balozi wa mazingira na muhamasishaji, Ndugu Michael Msechu, amekutana na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti, ambapo wamejadili mpango wa kufanya ziara ya kuhamasisha vijana na wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.
Amesisitiza kuwa kushiriki katika mchakato huu ni hatua muhimu kwa maendeleo ya taifa. Pia, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais kwa kuwa mabalozi wa maendeleo katika jamii.