the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 395
- 570
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mjini, Mhandisi James Jumbe Wiswa, amechangia mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga.
Mhandisi Jumbe amekabidhi mifuko hiyo ya saruji wakati wa ziara ya Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, ambapo wamekagua maendeleo katika Kituo cha Afya Kambarage na ujenzi wa barabara ya Kenyatta-Karena kwenye kata hiyo.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mifuko ya saruji, Mhandisi Jumbe amesema, “Nimeamua kutimiza ahadi yangu kutoa mifuko hii ya saruji ili kuimarisha ulinzi katika Kituo cha Afya Kambarage. Kamati ya Kituo hiki iliniletea ombi la kuchangia ujenzi wa uzio na mimi nimelijibu kwa vitendo. Kituo hiki kipo kwa ajili ya wagonjwa mbalimbali na wengi ni akina mama na watoto, na tunahitaji kuwalinda kwa kila hali.”