Wakuu hivi ni vijisent alivyovibakiza bank za Bongo tu!
Hebu tujiulize vijiswali vidogo vifuatavyo:-
Je a/c zake nje ya bongo za dola, euro, Yen ..... zitasoma sifuri ngapi?
Je shambani kwake kafukia kiasi gani (Km yule mjomba wa Zambia)?
Je tukichunguza investments alizonazo e.g majumba, magari, vijisenti vilivyoko kwenye a/c ya mkewe, wanawe, nduguze na marafiki wa karibu itakuwa na thamani gani?
Huyu ni mmoja tuliemgundua kwa bahati mbaya, je ni wangapi wanaomiliki mihele kama hii ktk nchi yetu?
Je unafikiri vibakuli tunavyovitembeza kwa wafadhili vyote vinamiminiwa kwenye vipaumbele vya kitaifa au vinamiminiwa mifukoni mwa wenye mkono mrefu wa kuchukua chao mapema?
Je x...........?
Kweli hii ndio nchi ya WADANGANYIKA! Kindly M4C help us ......!