Nimechukua jukumu la kufuatilia kwa karibu kujua ni mhasibu gani pale Hazina anaweza kuwa na kiasi kikubwa cha pesa kiasi kile. Habari zilizopo ni kwamba inasemekana mlengwa ni Mhasibu Mkuu wa Serikali anadaiwa amekuwa akichota pesa nyingi kwa njia ndogondogo lakini nyingi sana ikiwemo kuwalazimisha watu waliochini yake kumuweka(yeye) katika malipo ya posho kwa kila shughuli inayofanyika pale ofisini na amekuwa akilipwa kwa kila shughuli maalumu kama msimamizi mkuu wa shughuli bila kujali yupo ofisini, yupo nje ya nchi au yupo likizo.
Inasemekana viposho mbalimbali anavyolipwa kwa mwezi kutokana na shughuli za pale ofisini kwake zimekuwa zinamuingizia zaidi ya milioni80 kwa mwezi inadaiwa kwamba proposal yeyote ya kazi isiyo onyesha posho yake itakuwa bei gani haiwezi ikapita kirahisi. Inasemekana hilo siyo suala linalowakera sana kinachowakera sana ni kile kitendo cha kuwabana sana kimaslahi watu walio chini yake na kuwafanyia roho mbaya mbaya zisizo na mbele wala nyuma, "imefikia
mahala utasikia Mhasibu mkuu wa Serikali ana mgogoro na mtu mdogo kama secretary au dereva fulani na kamhamisha kituo cha kazi na kufuatilia aliko mhamishia kama anapata taabu kama alivyokusudia au lah, shughuli ambayo kimsingi hatakiwi kuisimamia mtu wa hadhi yake".
Taarifa zinaendelea zaidi kwamba kutokana na kwamba mkataba wake wa kazi karibia utaisha ameongeza ukali(orally) kwa watu wanaomuwekea viwango vidogo vya posho kwa kisingizio cha ufinyu wa bajeti kwa kila shughuli hivyo inahisiwa ana mabilioni ya Shiringi katika akaunti yake ambayo watu wa chini yake wanaweza wakawa wametoa hii chokochoko ili Serikali imchunguze na iangalie vyanzo vyake iweze kubaini posho anazo saini hata akiwa likizo, na vishughuli mbalimbali anazozianzisha ilimradi tuu yeye apate pesa. Kuna taarifa pia kwamba kwamba kaanzisha viproject vingi sana vya ujenzi lakini vina maslahi yake kama vile ukarabati wa kisehemu kidogo cha kukaa wastaafu wakisubiri huduma, inadaiwa kimeghalimu Milioni58 na hiyo kazi imefanywa nayeye akishirikiana na mtu wake wa karibu sana (Afsa utumishi) bila kuwa shirikisha watu wa ugavi, kuna mtu anaifanyia finishing hii kashfa ataileta hapa jamvini soon.