Mhasibu wa Chuo cha Nyuki Tabora ashtakiwa kwa makosa 9 ikiwemo Uhujumu Uchumi

Mhasibu wa Chuo cha Nyuki Tabora ashtakiwa kwa makosa 9 ikiwemo Uhujumu Uchumi

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Taasisi ya Kuzuia na Kupambambana na Rushwa (TAKUKURU) imemfungulia kesi Leonard Wilson Chishomi katika Mahakama ya Wilaya ya Tabora mkoani humo kwa makosa ya kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri kinyume na Sheria.

Makosa mengine ni Ubadhirifu na Ufujaji wa Mali ya Umma kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa pamoja na Kugushi Nyaraka na kujipatia kiasi cha Tsh. Milioni 6.43.

Mhasibu huyo alisomewa mashtaka mbele ya Hakimu wa Wilaya, D.S .Nyakunga ambapo alikosa dhamana na kupelekwa Gerezani. Kesi imeahirishwa hadi Aprili 20, 2023 itakaporejea kwaajili ya kutajwa.

TAKUKURU TABORA
 
Takukuru inashughulika na vidagaa TU

Kesi ya mil 6 wanaitisha Hadi press conference

Wakati Kuna mapapa yametajwa ripoti ya CAG yamekwapua mabilioni wa walipa kodi yanatamba mitaani.

Hi nchi Sijui alieturoga nani

Hovyo KABISA[emoji3525]
 
Uyo mhasibu nadhan atakua ndo wale wahasibu junior njaa Kali wagonga mihuri.

kachukua mkopo wa mil.6 kwa dhamana ya mwajiri wake,kaacha kazi kaingia mitini.

Hakuna mhasibu mpuuzi ,
Tena wa chuo kabisa anaweza kupiga dili la mil 6 eti mpk lfikie limharibie kazi.

Otherwise
Kuna namna uyu kijana anakomolewa[emoji4]
 
Siku hukumu ikitoka muje mtwambie pia maana hamna uwezo wa kishinda
 
DPP wa Magufuli anakamatwa lini

Huyo muhasibu apewe plea bargaining kama mafisadi
 
Back
Top Bottom