Mhaya akichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania, akienda kuhutubia UN mambo yatakuwa hivi

Mhaya akichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania, akienda kuhutubia UN mambo yatakuwa hivi

Rozela

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2024
Posts
845
Reaction score
2,235
Ndugu marais hamjambo (kwa lafudhi ya kihaya), naona wengi wenu mnashida sana, mfano we Trump hutulii kabisa, nimeamua kukupa msaada wa dhahabu tani 1 bure, Tanzania ni Tajiri hatuna njaa.

Halafu we Putin inaelekea huna kazi ya kufanya, ntakuletea Tanzanite utengeneze urembo uuze upate hela. Ona Zelensky alivyo konda, anahitaji msaa kwakweli, jioni ntaagiza gunia 100 za almasi auze ajenge nchi yake.

Nyie wazungu mnaonekana mna shida sana, ntakuwa nawasaidia. Ngojeni kwanza nimalize kujenga ikulu Bukoba, Bukoba mnaijua nyie au mnaishia huku maporini New York.

Njooni Bukoba mpate exposure. Halafu kuanzia leoziwa Vicroria litaitwa Rutashobya, aliyeligundua ni Mhaya sio mzungu, hata hapa America Wahaya ndio walikuwa watu wakwanza kuishi.

Elon Musk ni mhaya, Mark Zuckerberg ni Mhaya, Rick Ross ni mhaya, Jay Z ni Mhaya sema hawataki tu kujitambulisha kama ilivyokuwa kwa Obama na Camara Harris au yule Martin Luther King Jr.

Mwisho nataka kuwauliza hotel kali kuliko zote iko wapi nataka kuleta mbuzi wangu vacation. Asanteni.
 
Mods: kwenye title nilimaanisha kuhutubia.
 
Back
Top Bottom