Abuka
JF-Expert Member
- Sep 17, 2013
- 248
- 242
Tarehe 16/03/2019 Waziri mwenye dhamana ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo la Makazi Mhe William Lukuvi alizindua zoezi maalumu ya kutambua Kila kipande Cha Ardhi katika Mkoa wa Dar es salaam na kutoa Leseni za Makazi.
Katika mkutano wake na waandishi wa Habari pamoja na viongozi wote wa Mkoa wa Dar es salaam, Lukuvi alisema mwananchi atatambuliwa na baadae atatakiwa kuchangia sh. 5,000 ili kupata Leseni ya Makazi.
Lukuvi alisema katika hiyo 5,000, shilingi 4,000 zitagharamikia uandaaji wa Leseni na katika shilingi 1,000 inayobaki, 700 atalipwa mtaalamu anaezunguka kufanya utambuzi kwa kila Nyumba na 300 atalipwa mjumbe anaezunguka na huyo mtaalam.
KINACHOENDELEA
Baada ya uzinduzi huo, wanafunzi kutoka Chuo Cha Ardhi Morogoro walipewa hiyo kazi ya kufanya utambuzi. Wanafunzi hao walipangiwa kata mbali mbali za Dar es salaam ambapo iliwalazimu kutoka Morogoro na kwenda kupiga kambi ikiwemo Kupanga Nyumba za kuishi.
Wiki ya Pili Sasa wanafunzi hao wanaishi kwa gharama Yao wakisubiri vifaa vya kufanyia kazi (yaani simu janja), kwa bahati mbaya pamoja ya kulipia Nyumba mwezi mzima, wameanza kuhamishiwa kata nyingine kwa kisingizio Cha kata haihusiki na mradi huu. Mfano Watu waliopangiwa na wizara kufanya kazi kata ya Mbweni (wameshalipia gharama za maisha huko) Sasa wanahamishwa na hiyo hiyo wizara kwenda Makumbusho.
UTATA
1. Waziri alitangaza wanafunzi watalipwa shilingi 700 kwa parcel moja, uhalisia Ni kwamba wanafunzi walikuja kutangaziwa kwamba wao wanatakiwa kulipwa sh 400 na sio 700 Kama Waziri alivyotangaza (eti Waziri hakuwa updated)
2. Hao wanafunzi hawalipwi kwa siku inayopotea, wanalipwa kwa idadi ya Nyumba wanazofanya kwa siku. Kwa maana wanafunzi wamepoteza wiki ya Pili Sasa wakisubiri vifaa vya kufanyia kazi na hata waliopata vifaa wamepata vifaa nusu. Inamaana mpaka Sasa hawajaingiza pesa yoyote Bali wametumia tu.
3. Tunajua kwamba Kuna zoezi la urasimishaji linaendelea huko mitaani, makampuni yanayopima yanahamasisha watu kujiunga kwa pamoja ili kuchanga pesa (sh 250,000) za upimaji.
Mwananchi akipata Leseni ya Makazi ataweza kuitumia Kama Hati kwa muda wa Miaka 5, ndani ya muda huo anatambulika rasmi Kama mmiliki, Anaweza kuomba mkopo akakopesheka, na zoezi la Leseni za Makazi Ni bure. Hii imepelekea wananchi wengi kukimbilia Leseni za Makazi na kusukumia mbele zoezi la upimaji, kwa namna nyingine kwamba Sasa wananchi wana Miaka mitano kuhakikisha kwamba wamepima, haiwalazimu kuendelea sahivi.
Kampuni za upimaji, zinakutana na changamoto ya kutopewa kipaumbele na wananchi, hivyo chakula Chao kudorora.
HUJUMA
Kampuni za upimaji zimeamua kuungana na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara kukwamisha zoezi. Kampuni zinatoa ahadi nzito na wenye Mamlaka kuitangaza kwamba Kata Fulani hakuna kazi, kampuni ya upimaji imejipanga kukamilisha kila kitu na Kisha kuwahamisha wanafunzi kata nyingine ilimradi kuwapotezea muda
ANGALIZO
Kumbuka hao Ni wanafunzi ambao wametumia muda wao wa mazoezi kwa vitendo kufanya hili zoezi na kwamba muda wao wa kurudi Chuo ukifika watalazimika kurudi chuoni hata Kama zoezi halijakamilika.
Hii ni namna ya kuwapotezea muda wanafunzi ili muda wao wa kurudi ufike, na zoezi lishindikane.
USHAURI
Agizo litoke kila mmiliki ambae Hana Hati aweze kupata Leseni za Makazi.
Kama tayari yupo kwenye Mpango wa urasimishaji na amewekewa beacon/mawe/mipaka asihusike. Lakimi wote ambao hawajawekewa beacon/mawe wapewe Leseni za Makazi huku wakiendelea na urasimishaji
Zoezi la Leseni za Makazi halizuii zoezi la Hati.
Asanteni Sana
Chanzo: Mjumbe Chamanzi.
Sent using Jamii Forums mobile app