Fundi Madirisha
Senior Member
- Jun 30, 2020
- 184
- 988
Amani iwe juu yenyu wanajukwaa!
Mimi nataka kujua, hivi katika hii kesi ya Mbowe mnufaika ni Jamhuri au CCM? Nauliza hivi kwa sababu najaribu kutazama kwa jicho la mbali ni kwamba, Mhe Mbowe hana records mbaya za kuisumbua serikali na wala hajawahi kulazwa jela kwa matukio ya utovu wa kinidhamu zaidi ya siasa tu. Sasa kwenye hii kesi yake mnufaika ni Jamhuri au CCM? Kama ni hivyo, CCM watanufaika na kipi Mbowe akiwa Jela?
Sina mjadala na hasara watakayoipata CHADEMA Mbowe akifungwa jela ingawa wao wanaweza kuchukulia poa, huyu ni Gwiji wa siasa za upinzani nchini, nadhani ukimtafuta mtu wa aina yake CCM labda unaweza kumpata Mzee Mangula, JK, Kinana na Lowasa. Lakini kiwatoa wazee hawa ambao umri wao umeshakimbia,hakuna CCM mwingine wa kumfikia Mbowe.
Hivyo ni lazima tukubaliane kua Mbowe awapo Jela CHADEMA kitatetereka sana na nafikiri hii ndiyo shabaha kuu ya kesi hii. Mbowe ni sponsor, ni leader, Ni motivator, ni educators, ni mentor, ni great thinker,ni decision maker. Hakuna ahueni ndani ya CHADEMA Mbowe awapo Jela.
Naripotia kutoka msitu wa Mbao Uhoro-Rufiji
FUNDI MADIRISHA.