Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mhe. Njalu Silanga, Mbunge wa Jimbo la Itilima
Mhe. Njalu Silanga, Mbunge wa Jimbo la Itilima tarehe 05 Mei, 2023 alipata nafasi ya kuchangia suala la Tanga Cement na Twiga Cement wakati wa kuwasilishwa kwa hoja ya bajeti ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara iliyosomwa na Waziri mwenye dhamana Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
"Ni vyema serikali itueleze ni jambo gani limejificha katika #SakataLaTwigaCementTangaCement ambalo wananchi na wabunge hawafahamu ili mwisho tuwekane sawa" - Mhe. Njalu Silanga, Mbunge wa Jimbo la Itilima
"Wafanyabiashara wanapoongezeka ndivyo ushindani unaongezeka, lakini pia ikumbukwe tunajenga barabara, mashule, sasa najiuliza kama viwanda vinaongezeka na huyu Tanga Cement anataka kuuza hisa zake na sijui anamuuzia nani. Na kama serikali ina mpango mzuri basi mashirika yenu ya umma yaungane ili kununua hisa hizo za Tanga Cement ili nyinyi mmiliki na muondokane na hii sintofahamu iliyopo hivi sasa" - Mhe. Njalu Silanga, Mbunge wa Jimbo la Itilima