Elections 2010 Mhe. Rais hajui athari za kauli zake...

teheee yale maji ya kilimanjaro mbona yalikuwa kama lemon vile?
 
Mheshimiwa Rais anajua fika kuwa uchaguzi ujao uko mikononi mwa wafanyakazi. Kilichompa kiburi ni woga wa kudhani kuwa ikiwa wafanyakazi watagoma basi atashindwa kabisa kuwanyamizisha. Kwa hiyo suluhu lake kwa muujibu wa Rais ni kutumia "UNYERERE", vitisho ndio lugha pekee. Mnakumbuka pale chuo kikuu cha Sokoine kilipojiandaa kugoma wakati Mwl Nyerere alipokuwa Mkuu wa chuo hicho.

Kwa Rais na washauri wao wanatangaza huo kama ushindi, kwani wafanyakazi hawakudiriki kujitokeza katika maandamano, na madai yao yakazikwa. Hilo ndilo lilikuwa lengo fupi la Mheshimiwa Rais. Kuhusu uchaguzi, hilo ni swala la kesho ambalo mheshimiwa Rais kwa kuwafahamu fika watanzania anajua kuwa atavuka kikwazo hicho. Si mnajua kuwa watanzania wanaweza kugeuzwa kwa kipindi cha miezi miwili. Kwa kuelewa hili mheshimiwa Raisi hana hata tumbo joto kwa vile Doze ya hiyo homa anayo.

Swali la msingi ni nini kitafuata kwa Wafanyakazi wanaopata mshahara kiduchu? Mchezo ndio umekwisha au ndio wana kwanza unaanza? Hivi ni nani aliyeshika kwenye makali Wafanyakazi au ni Raisi? Hayo ndio maswali muhimu ya kujiuliza umoja wa wafanyakazi kabla ya uchaguzi mkuu. Moja kati ya maswali hayo, jibu ni nalo kuwa mshahara hautoshi si siri. Ila hili la ufumbuzi ni kitendawili tega.

Wakati tunasubiri maoni ya uongiozi wa chama cha wafanyakazi, watanzania bado tunajiuliza hivi ni wapi tunakwenda. Kuna chama kingine zaidi ya CCM kinaweza kuja kutatua swala la mishahara vizuri zaidi. Na kama kipo ni chama gani?
 

Mdau, nakubaliana nawe katika hoja hii ya staili akiyotumia Mhe. Rais kuwanyamazisha wafanyakazi. Hata hivyo, twende mbele turudi nyuma bado hata wale wanaomsahuri akurupuke nao ni wafanyakazi wa nchi hii na wasome pia alama za nyakati. Yote ambayo wajaribu kuyafunika ni madhara yake ni makuu kwao na kwa vizazi vya vijazo.

Suala la kwamba hakuna chama ambacho kinaweza kulatea mabadiliko ya kweli nadhani sasa iondoke katika vichwa vyetu, tukiwaza kama wote tuna ndoa ya kidini na CCM na kwamba dini hairuhusu kuvunja ndoa, manake tufubiri mpaka kifo kitakapotutenganisha na huyo CCM na hapo tutawaacha watoto wetu na vizazi vyao ili nao waamue juu yetu.
Kwani hakuna aliyejifunza kuwa nchi hii mtu yeyote anaweza tu kuiongoza ?? kwani hatujui kuwa tumekuwa tukibahatisha kuchagua hao watawala ambao tunadhani wanaweza na hakuna wengine milele?.

Binafsi nadhani mtu ambaye huwezi kumkataa na kuachana nae maishani ni mzazi wako ambaye hata ukimwacha kinadhalia, bado dhamira yako itakukumbusha kuwa yeye ndie aliyekufanya wewe huwpo hapa duniani. Siona kama hakuna wengine wanaoweza kuiongoza inji hii kama staili ya uongozi wenyewe ndo huu tulionao labda kama watendaji wa Serikali (ambao ndo muhimu) watagoma kumtumikia kiongozi wingine zaidi wa kutoka CCM!.Tujifunze kutoka kwa mataifa ya wenzetu ambayo kila siku tunaona wanalazimisha mabadiliko .....huu woga wa kuamua ndio unaotufanya tuonekane mabwege kila kukicha na tutaendelea hivyo milele.
 

Hata kama TUCTA ni wazushi; thats not a way a president of the Republic should conduct himself; Tulio wazazi tunajifunza kuwa humwonyi na kumshauri mtoto kwa kejeli na dhihaka na mijishasira na vitisho.......... UNASHINDA NAE?
 
JE KIKWETE ANAAMINI KATIKA NGUZO TATU ZINAZOTAWALA NCHI ANAYOIONGOZA
Nashukuru kwa tanbihi iliyotolewa hapa juu na Ngoshwe analysis yake inaweza kuamsha ari ya wafanyakazi kudai zaidi haki zao. Kiongozi wetu amekosea na zaidi kosa lake ni kuruhusu maelezo ya wapambe wake wa toka kampeni za uchaguzi 2005 kuendelea kumlaghai. Kikwete pale amefanya kosa la kihistoria kwa kubagua hadhira ya demokrasia (wafanyakazi wa UMMA), kama kiongozi wa nchi hisia hizo angezificha kwani hao waomba kura mara ngapi wanaficha mambo ambayo huwa hawaamini lakini ili kufanikisha anapata kura yake anayamezea.

Je, si fedheha kwa kiongozi wa nchi kama yeye kukiri hadharani kuwa uwezo wa serikali kwa miaka minane ijayo haiwezi kuongeza pato lake la sasa? Kama kiongozi amekwisha kukataa tamaa kwamba kwa vyo vyote vile hawezi kuikwamua hiyo nchi kwenye tope iliyoinasa WATOZA USHURU WETU ya kushindwa kubuni mbinu za kuibua vyanzo vingine vya mapato zaidi ya kutegemea ushuru wa kwenye vibaraza, je si ingekuwa busara basi akaegesha hilo STK pembeni na kuwaruhusu wenye MAONO wampokeee. Malalamiko ya kuwa na mapato kidogo hayapaswi kusemwa semwa na mkubwa, jemedari siku zote anakomalia kwenye FIKRA ZILIZO HAI hata kama anaona njia ya kujikwamua inamagumu, atawahakikishia wafuasi wake kuwa watafanikiwa kuvuka kikwazo kilichoko mbele yao.

Mie nadhani mkubwa mwisho wa mwezi huu ajitokeze tu kwenye KIOO aweze kuwasihi tu wafanyakazi kuwa hakuwa na maana hiyo inayotafsiriwa na mwandishi huyu na wengine kama yeye, MKUBWA HAAMBIWI KAJAMBA, na kwa desturi ya watanzania wanavyo kubali majibu marahisi marahisi kama walivyowakilishwa na vijizee vya BONGO kwa kupiga makofi hata pale walipoambiwa nchi ni maskini ,watamsamehe na kumpa ushindi wa kishindo isipokuwa iiiiiiiiiiiiiiii.

Kusema kwa ujeuri na kejeli kuwa atawafukuza watumishi walio chini yake, je, na rahisi kama tamko la kisiasa, kuwa nakufukuza, nadhani mihimili ya dola ipo katika kutulinda sote, yeye na sisi, kusema mgomo ule ni batili yeye hana mamlaka ya kutoa tamko hilo, bali ni mahakama, au ni yale yale kuwa yu juu ya sheria, hiyo si kweli,je kama mkubwa amekanyagia chini mhimili moja wa dola, tutakuwa na imani gani naye tena.

Naomba WTZ wajihi, sifa na uledi wa watu wa IKULU na wale wanaomshauri Rais siku hadi siku, nina mashaka nao, inawezekana hao watu wanachukulia Rais kama kirafiki fulani hivi, kidogo inanichanganya, Rais ni TAASISI kwahiyo anapokuja kutoa hoja, hoja yake inabeba taasisi nzima (washauri wake wote kwa nafasi na majukumu yao) sasa Hotuba ile sijui nani kaiandaa, nilishutshwa na RAIS kutaja jina la mwananchi ambaye anaongoza taasisi, hiyo kwangu ni mapangufu, imeitia familia ya mwananchi yule kwenye mashaka, ndiyo, ni nani anaweza kuishi maisha ya utulivu huku unasimangwa na RAIS, embu niambieni, mwokozi wake ni mhimili mwingine wa dola nadhani ndo inaweza kumhakikishia usalama wake.

Niweke koma kwenye maoni yangu kwa kusema kuwa maneno ya Rais yamemchonganisha yeye na wafanyakazi wanaomsaidia katika shughuli zake za kila siku na kingine kibaya zaidi, wafanyakazi wamechonganishwa na wananchi na MKUBWA mwenyewe, kusema wafanyakazi wanataka fedha za madawa na maji yanayolengwa kwenda kwa mwananchi, watu vijijini na wengine wataamini maskini ya mungu. TAFAKARI
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…