Mhe. Rais uliyoyaona Morogoro Manispaa yako Ofisi zote za Serikali

Mhe. Rais uliyoyaona Morogoro Manispaa yako Ofisi zote za Serikali

Patriot

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Posts
5,705
Reaction score
4,703
Maafisa wa manispaa ya Morogoro wamejimilikisha ’vizimba’ na kupangisha upya kwa gharama ya juu! Kwa ujumla kilichotokea Morogoro ni matumizi mabaya ya ofisi ambayo ktk serikali, yako kila sehemu.

1. Ukiwa Afisa Ardhi, unapima viwanja na kujimilikisha viwanja vingi ili uwauzie wengine.

2. Ukiwa afisa wa Wizara ya Elimu, unajenga shule nyingi watoto wako unawapanga shule nzuri zenye waalimu wa kutosha.

3. Nyumba za National Housing zinachukuliwa na maafisa halafu wanazipangisha upya kwa wengine.

4. Ukiwa waziri wa ujenzi unatangaza tenda kampuni yako ndo inapewa kujenga mradi.

5. Ukiwa daktari unafika muhimbili kusikiliza wagonjwa wa kifua, halafu unawaelekeza kwenye duka lako la dawa au mashine yako ya vipimo vya kichwa hapo Upanga.

6. Ukiwa afisa wa TCU au mikopo ya elimu ya juu unawapangia watoto wako masomo wanayoyataka na mikopo, wengine unawalazimisha na hata kuwanyima mikopo.

7. ......................etc.
Tusemeje sasa? Manispaa walikosea lakini ni kila sehemu ni uozo.
 
Yote hayo anayafahamu vizuri sana ila huwa anajifaragua mbele ya hadhara ili aonekane amegundua na ni mapya kwake!
 
Ukiwa RTO daladala zako hazitii sheria za barabarani wala madereva wake kuwa na leseni sahihi kwa ajili ya kuendesha abiria
 
Very unethical behaviour. Ardhi ilikuwa balaa. Viwanja ukiona 10 elfu, basi a sizable portion has been retained by same people that invite the public to buy the plots
 
Yeye mwenyewe alifanya hayo hayo kwenye uchaguzi kwa kuagiza yeye binafsi na wagombea wenzake wa CCM watangazwe washindi kwa shuruti. Kimsingi unaripoti tatizo kwa mtu ambaye ni sehemu ya hilo tatizo.
Tena yeye ni tatizo zaidi
 
Hana atakachokifanya ataishia kufura tuu,pili huko maofisini wako wtu kama walio nje ya maofisi wana ego kama za wengine
 
Kufa kufahana, hii yote ni selfishness or self-centered spirit most of our leaders are too much of themselves
 
Ni vibaya kwa rais kuona mtendaji anafanya makosa kama hayo ya watu wa Morogoro, unatoa maagizo hayo tu badala ya kuichukuwa kama somo kwa nchi nzima na sekta zote! Alistahili mara moja kutoa maagizo kwa nchi nzima kwa watumisihi wote wanaojinufaisha.
 
Ukiwa RTO daladala zako hazitii sheria za barabarani wala madereva wake kuwa na leseni sahihi kwa ajili ya kuendesha abiria
Hii tena ndo kiboko! Kila gari ya askari mwenzao wanaifahamu na wanapeana mikono tu, bila kujali ubovu wake.
Imefikia hata askari akiua mtu wanahangaika kumuondolea kosa kwa kupindisha uchunguzi.
 
Huko mbele watamuona Kama kikaragosi au mwanasesere hawamuogopi Tena

Kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake
 
Back
Top Bottom