Mhe. Waziri wa Afya, vitendo vyakupiga picha kwenye vituo vya afya na hospitali vimekithiri, faragha za wagonjwa zilindwe

Mhe. Waziri wa Afya, vitendo vyakupiga picha kwenye vituo vya afya na hospitali vimekithiri, faragha za wagonjwa zilindwe

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Watu wanafika hospitali, wanapiga picha wapendwa wao na watu wengine wanowazunguka bila ridhaa ya wale waliopigwa picha, hii si sawa.

Madaktari wapo kazini, baadhi ya wahudumu wa afya wasio na maadili wanarekodi video na kupiga picha kwa maelekezo ya ndugu wa mgonjwa au utashi wao tu..hii si sawa.

Waandishi wa habari wanakwenda maeneo ya kutolea huduma wanakuta wagonjwa wamelala au wapo foleni then wanarusha bila hata kuwaomba ruhusa wagonjwa husika ..hii si sawa.

Tupige marufuku huu utaratibu, tuweke sheria ya kushtaki mtu atakarekodi video na kuisambaza bila ridhaa ya wahusika, Jamhuri imejilinda kisheria, wagonjwa nao Wapewe nguvu ya kujilinda kisheria.

Watu waliopo hospitalini walindwe, tusiwadhalilishe. Mwisho sipendezwi na haya matangazo yanayoendelea kuhusu kipimo kipya cha COVID, yanaondoa utu na ni kinyume kabisa na maadili....picha za uchi za watu wakiwa wamelela kifudifudi wakisubiri kupimwa COVID zipigwe marufuku.
 
Mbona viongozi wa Serikali wakiwatembelea wagonjwa wanapiga nao picha na tunaziona luningani na magazetini?!
 
Mchezo huu umekithiri kwa vijana wa ufipa kwa kudhani serikali ya awamu ya tano itaondoka kwa mtindo wa picha!
 
Unakuta mgonjwa mwenyewe kabomoka mguu anauselfie

Then utaskia

Pray for me
 
Mchezo huu umekithiri kwa vijana wa ufipa kwa kudhani serikali ya awamu ya tano itaondoka kwa mtindo wa picha!
Kila kitu si cha kuweka politics man. Hoja ya wazir ni hoja nzuri sana. Lakin ziharibiwa na watu kama nyie ku include siasa kila mahali.
 
Mchezo huu umekithiri kwa vijana wa ufipa kwa kudhani serikali ya awamu ya tano itaondoka kwa mtindo wa picha!
Umepewa cheo gani awamu hii maana naona nguvu ya kupiga kelele kwa mfalme imeongezeka ghafla.
 
Back
Top Bottom