Kuna heshima na heshima. Wakati nchi nyingi za Kiafrika zinapata uhuru miaka ya 1960 Waingereza waliwapachika viongozi wengi waliokuwa wanawaachia madaraka UDOKTA. Kulikuwa na Dr. Nyerere, Dr. Obote, Dr. Kaunda, n.k. Hii ilikuwa ni fix ya kuwalainisha kwa kuwavika vilemba vya ukoka ili waendelee kuwa watiifu kwao. Baada ya muda viongozi wenyewe walibaini hilo na kuacha kutumia hizo heshima bandia. Kwa Mwalimu Nyerere alikwenda mbali zaidi na kuzuia kuitwa mheshimiwa au mtukufu na badala yake akapendekeza NDUGU. Mwalimu ilikuwa profession yake. Hizi DOKTA zinazosakwa na wanasiasa wetu sasa ni ulimbukeni tu. Hata ambao hawakuwahi kukaa darasani zaidi ya miaka 8 nao sasa ni madokta. Inashusha heshima ya madokata wakweli kwa sababu haitakuwa rahisi kubaini wa kweli na feki. Angalao mtu angekuwa anaonyesha dalili za u-intellectual kidogo labda tungemezea lakini wengine mmmhhhh! Hivi nani aliwahi kuona andiko lolote la Kikwete, iwe makala gazetini, mchango katika jarida au kitabu? Nani amewahi kuona andiko lolote la Karume? Lakini sasa ni madaktari!!!!!!! Kuna na wale ambao wameshtumiwa kughushi shahada na wao hawakukanusha tuhuma hizo lakini bado watu (hata waandishi wa habari na vyombo vyao) wanaendelea kuwaita MaDOKTA. Hivi kunyamaza si ushahidi tosha kuwa mtu amekubali tutuhuma? Tunapokuwa na marais au viongozi wa sampuli za kina Dr au Professor Maji Marefu kwa kweli ni tatizo kubwa. Labda itatusaidia katika Soko la Pamoja la Afrika Mashariki. Na sisi tutaonekana tumo ingawa hatuvumi.
SAWA MIMI SIO MWANASIASA ,.Vyuo vikuu vina Mathamanisho yake,..ya kiheshima either unaufuata MTAALA na unatunukiwa heshima baada ya kuumaliza, au Uthamanisho wa heshima unakufuata kutokana na mchango wako katika jamii,.ile vita ya kenya kwenye na baada ya Uchaguzi iliuwa si Ndogo,.wenyewe wanaelewa,..
publications mzee ni muhimu zinaweza kukugusa indirectly kutokana na uliyoyafanya ambayo yanaweza kutumika kama hadidu sehemu nyingine .,hiyo pia ni publication,.na inakubalika,.
mimi sio mwanasiasa ..
SUALA LA MAPROFESA hebu tuliangalie.,.ningependa tuzungumzie wa TANZANIA upande wa tiba[madaktari] NI VIPI WAMEWEZA KUWA MAPROFESA BILA KUWA NA PhD,..kwa walio wengi ninaowajua hawana Phd,.. Hawajawahi kuwa maasosiate PROF,..Lakini wanatambulika hivyo wakati ki mtaala haiko hivyo,.neno kubwa ni kupablish kupablish,.ameshapablish.,.. teaching staff,..teaching hours amefikisha point,.ni nani mwenye kuwahakiki?
Kwa huku tulipo ili upate masters DEGREE lazima upablish angalau pepa moja yenye mahusiano na tafiti yako ,.lasivyo humalizi shule,.na kama una uwezo basi zaidi ya hapo[motisha pia hutolewa kwa kila pepa inayotoka], KWA watu wa PhD pepa moja yenye mahusiano na tafiti yako tena lazima itoke SIC journal ,la sivyo humalizi shule,..je baada ya kufanya hivyo nikirudi bongo nitaitwa prof,.
lakini mbona wale wa BONGO wanaitwa maprofesa???
Basi ujue lazima kuna system ya vyuo vikuu ambayo imekubaliana na hali hiyo.,.ingawa wakija maprofesa toka nje majamaa huona noma na kujiita madockta.,lakini heshima ni heshima tu mzee ni kama tuzo ya NOBELI.,WANAKUBALIKA,.Ndio System ya dunia WAMEPEWA HAO TUZO YA KIDAKTARI,huna budi kukubali