Mmmh, sasa hizo si wanapewa wengi tu, mbona yeye yake inavuma kupita kawaida? Hadi kwenye mbao za ufunguzi wa majengo au shughuli fulani za kitaifa anaandikwa Dr. Sasa hii siitaleta shida baadaye kwa vizazi vijavyo watakapokuwa wanaona document zimeandikwa Dr au mbao za ufunguzi wa majengo zimeandikwa Dr, watajua Tanzania iliwahi kuongozwa na PhD holder. Confusion!!
Lakini pia PhD za hivyo Mkapa anazo kama tatu hivi na hakuwahi kuitwa Dr. Inasemekena Rais wa India kwa mfano, ni Professor lakini hata siku moja haitwi Prof. nk nk nk. Hii kitu inanipa shida kidogo.....
Lakini kwa kweli hapa kuna issue ya kuzingatiwa, maana udaktari wa namna hii huweza kuwa revoked. Sasa kama initials zimeenda kwenye mabango yaliyo permanent hapo itakuwa kasheshe.Huo ni ulimbukeni wake tu! Nyerere alikuwa nazo kama 12 hivi! Siku wakizihitaji sijui tutaanza kufuta hayo majengo yaliyoandikwa Dr. Mgabe wamechukua karibia zote!
Tatizo rais wako si mkwere au hujui inawezekana ana engineer mwenyewe iandikwe hivyo ,maana dr za namna hizo wengi wanazo ila hawaoni hekima kutumia...Nyerere alikuwa nazo ila huoni kutumika .
Jamani tusaidiane; Dr. ya Kikwete inamaanisha Daktari wa Falsafa yaani PhD (Alisoma wapi na lini?), Daktari wa binadamu au Daktari wa wanyama? Lakini kumbukumbu zangu zinaonyesha alisoma uchumi UDSM? Sasa huu Udokta uliogain popularity kubwa kiasi hiki ni Udokta gani huo? Maana kama ni hizi PhD za heshima, nakumbuka Mkapa pia alikuwa nazo kadhaa, hata Nyerere aliwahi kupewa, cha ajabu hawakuwahi kuitwa hivyo.
Shida ipo kwa waitaji (wanaomwita Doctor) au ipo kwa muitwaji (anapenda kuitwa Doctor).
Kuna heshima na heshima. Wakati nchi nyingi za Kiafrika zinapata uhuru miaka ya 1960 Waingereza waliwapachika viongozi wengi waliokuwa wanawaachia madaraka UDOKTA. Kulikuwa na Dr. Nyerere, Dr. Obote, Dr. Kaunda, n.k. Hii ilikuwa ni fix ya kuwalainisha kwa kuwavika vilemba vya ukoka ili waendelee kuwa watiifu kwao. Baada ya muda viongozi wenyewe walibaini hilo na kuacha kutumia hizo heshima bandia. Kwa Mwalimu Nyerere alikwenda mbali zaidi na kuzuia kuitwa mheshimiwa au mtukufu na badala yake akapendekeza NDUGU. Mwalimu ilikuwa profession yake. Hizi DOKTA zinazosakwa na wanasiasa wetu sasa ni ulimbukeni tu. Hata ambao hawakuwahi kukaa darasani zaidi ya miaka 8 nao sasa ni madokta. Inashusha heshima ya madokata wakweli kwa sababu haitakuwa rahisi kubaini wa kweli na feki. Angalao mtu angekuwa anaonyesha dalili za u-intellectual kidogo labda tungemezea lakini wengine mmmhhhh! Hivi nani aliwahi kuona andiko lolote la Kikwete, iwe makala gazetini, mchango katika jarida au kitabu? Nani amewahi kuona andiko lolote la Karume? Lakini sasa ni madaktari!!!!!!! Kuna na wale ambao wameshtumiwa kughushi shahada na wao hawakukanusha tuhuma hizo lakini bado watu (hata waandishi wa habari na vyombo vyao) wanaendelea kuwaita MaDOKTA. Hivi kunyamaza si ushahidi tosha kuwa mtu amekubali tutuhuma? Tunapokuwa na marais au viongozi wa sampuli za kina Dr au Professor Maji Marefu kwa kweli ni tatizo kubwa. Labda itatusaidia katika Soko la Pamoja la Afrika Mashariki. Na sisi tutaonekana tumo ingawa hatuvumi.MWALIMU NYERERE BAADA YA UHURU ALIKUWA ANAJULIKANA KAMA Dr.Nyerere kote duniani,..mpaka baadaye,..sijui ilikuwaje akaanza kuitwa mwalimu,..au mwenyekiti .,.na Watanzania wote tukawa tunaitwa ndugu,.kulikuwa hakuna mtu anayeitwa mheshimiwa au mtukufu sio waziri hata mbunge.,..
kwa urusi wakati wa Ukomunisti raia wote walikuwa wanajulikana kama [matavarishi],kama ulikuwa na ushiriki kwenye chama pamoja na nafasi bosi wewe ni COMREDI,.
system duniani imebadilika ,..sasa ni MTUKUFU ,.mheshimiwa,..Hamana COMRADE wala NDUGU,..
ndio dunia hiyo,..KAPEWA heshima ya kuwa DK.,.na akainama KAMBA ya KOFIA ikabadilishiwa upande ,.ina maana alikubali hiyo heshima ,.sasa tatizo ni nini?
MIMI ni muumini WA NYERERE Mpaka MWISHO,...YOU DONT LOOK FOR Respect but you earn it.//na ukiipata basi ikubali.,.na huna budi kuitunza hiyo heshima mpaka mwisho.,..
Kwakweli hapo kwenye nyekundu ni changamoto. Nimeshangaa hata kwenye press release ya wahadhiri wa chuo kikuu na wenyewe wamemtaja kama Dr. Kikwete. Kuna haja ya kureview matumizi ya hili neno ili ijulikana linatumikaje na kwa maana gani. Kama vipi vyuo vikuu viache kutoa degree za aina hiii, bali zije na kitu kingine cha tofauti kitakachoonyesha kwamba ni heshima aliyopewa mtu na si kumwita Doctor ilihali hata hajui hiyo Dr. inasotewaje? Wafanye kama Malkia ambaye huwa anatoa "Sir". Sasa hivi layman hawezi jua tofauti ya Udokta wa Kikwete na wa Magufuli. Wakati in reality ni za mbali kama mbingu na nchi.Kuna heshima na heshima. Wakati nchi nyingi za Kiafrika zinapata uhuru miaka ya 1960 Waingereza waliwapachika viongozi wengi waliokuwa wanawaachia madaraka UDOKTA. Kulikuwa na Dr. Nyerere, Dr. Obote, Dr. Kaunda, n.k. Hii ilikuwa ni fix ya kuwalainisha kwa kuwavika vilemba vya ukoka ili waendelee kuwa watiifu kwao. Baada ya muda viongozi wenyewe walibaini hilo na kuacha kutumia hizo heshima bandia. Kwa Mwalimu Nyerere alikwenda mbali zaidi na kuzuia kuitwa mheshimiwa au mtukufu na badala yake akapendekeza NDUGU. Mwalimu ilikuwa profession yake. Hizi DOKTA zinazosakwa na wanasiasa wetu sasa ni ulimbukeni tu. Hata ambao hawakuwahi kukaa darasani zaidi ya miaka 8 nao sasa ni madokta. Inashusha heshima ya madokata wakweli kwa sababu haitakuwa rahisi kubaini wa kweli na feki. Angalao mtu angekuwa anaonyesha dalili za u-intellectual kidogo labda tungemezea lakini wengine mmmhhhh! Hivi nani aliwahi kuona andiko lolote la Kikwete, iwe makala gazetini, mchango katika jarida au kitabu? Nani amewahi kuona andiko lolote la Karume? Lakini sasa ni madaktari!!!!!!! Kuna na wale ambao wameshtumiwa kughushi shahada na wao hawakukanusha tuhuma hizo lakini bado watu (hata waandishi wa habari na vyombo vyao) wanaendelea kuwaita MaDOKTA. Hivi kunyamaza si ushahidi tosha kuwa mtu amekubali tutuhuma? Tunapokuwa na marais au viongozi wa sampuli za kina Dr au Professor Maji Marefu kwa kweli ni tatizo kubwa. Labda itatusaidia katika Soko la Pamoja la Afrika Mashariki. Na sisi tutaonekana tumo ingawa hatuvumi.
Kuna heshima na heshima. Wakati nchi nyingi za Kiafrika zinapata uhuru miaka ya 1960 Waingereza waliwapachika viongozi wengi waliokuwa wanawaachia madaraka UDOKTA. Kulikuwa na Dr. Nyerere, Dr. Obote, Dr. Kaunda, n.k. Hii ilikuwa ni fix ya kuwalainisha kwa kuwavika vilemba vya ukoka ili waendelee kuwa watiifu kwao. Baada ya muda viongozi wenyewe walibaini hilo na kuacha kutumia hizo heshima bandia. Kwa Mwalimu Nyerere alikwenda mbali zaidi na kuzuia kuitwa mheshimiwa au mtukufu na badala yake akapendekeza NDUGU. Mwalimu ilikuwa profession yake. Hizi DOKTA zinazosakwa na wanasiasa wetu sasa ni ulimbukeni tu. Hata ambao hawakuwahi kukaa darasani zaidi ya miaka 8 nao sasa ni madokta. Inashusha heshima ya madokata wakweli kwa sababu haitakuwa rahisi kubaini wa kweli na feki. Angalao mtu angekuwa anaonyesha dalili za u-intellectual kidogo labda tungemezea lakini wengine mmmhhhh! Hivi nani aliwahi kuona andiko lolote la Kikwete, iwe makala gazetini, mchango katika jarida au kitabu? Nani amewahi kuona andiko lolote la Karume? Lakini sasa ni madaktari!!!!!!! Kuna na wale ambao wameshtumiwa kughushi shahada na wao hawakukanusha tuhuma hizo lakini bado watu (hata waandishi wa habari na vyombo vyao) wanaendelea kuwaita MaDOKTA. Hivi kunyamaza si ushahidi tosha kuwa mtu amekubali tutuhuma? Tunapokuwa na marais au viongozi wa sampuli za kina Dr au Professor Maji Marefu kwa kweli ni tatizo kubwa. Labda itatusaidia katika Soko la Pamoja la Afrika Mashariki. Na sisi tutaonekana tumo ingawa hatuvumi.