Mikopo Chefuchefu
JF-Expert Member
- May 15, 2017
- 3,373
- 6,795
Kwanza nianze kwa kukupongeza jinsi unavyotimiza wajibu wako wa kuliongoza taifa hili kwa ufanisi mkubwa na wa hali ya juu.
Wewe ni mtu muwazi, unayepokea maoni ila ni kiongozi shupavu asiyeyumbishwa.
Tumeona msimamo wako thabiti kwa mfano katika jitihada zako za kuhakikisha watoto wa kike wanafika mbali kielimu. Japo mabeberu walidhani kwa kutumia visenti vyao wangeweza kukuyumbisha, hukuyumba hata kidogo... Watanzania wengi tupo nyuma yako katika hilo.
Sambamba na hilo, nilikuwa nimesukumwa kumpendekeza na kuleta maombi kwako kumfikiria ndugu Lazaro Mambosasa kwa nafasi ya ukuu wa jeshi la Zimamoto na uokoaji.
Ni mtu msikivu na muwajibikaji mwenye rekodi nzuri ya utendaji hivyo nadhani anaweza akatusaidia sana katika eneo hilo.
Natanguliza shukran zangu za dhati.
Wasalaam