Mheshimiwa Wasira umemwona Mheshimiwa Kigoda.... Fuata Nyao!!!

Mheshimiwa Wasira umemwona Mheshimiwa Kigoda.... Fuata Nyao!!!

Kimboko

Member
Joined
Nov 16, 2010
Posts
56
Reaction score
6
Nilikuwa napitia gazeti la mwananchi ya jana tarehe 5 March, 2013 kwamba mheshimiwa Kigoda ameipa rungu bodi ya TBS kufanya mabadiliko makubwa kwenye shirika la TBS, nami kama mdau wa biashara na maendeleo ya Nhci hii nakuomba uchukue hatua kama za mheshimiwa Kigoda kuzipa bodi za taasisi zilizo chini yako ikiwa ni pamoja na ya TASAF kufanya mabadiliko makubwa ikizingatiwa kuna ubadhirifu mkubwa sana hasa kwenye manunuzi katika taasisi hii. Tuma special audit uone ukweli wa mambo baba.

Vijana wako wamesimamishwa kazi,wanadai haki zao kisheria la kusikitisha kurugenzi ysa TASAF inawaandikia recommendatio mbaya ili tu wasipate kitu ambacho ni kinyume na sheria za nchi.

Kuna madereva wanadai haki zao za msingi kabisa na swala hili likokwenye vyombo vya sheria linafanyiwa kazi lakini Mkurugenzi wa TASAF ngugu Mwamanga anawafanyia ukatili ambao haupo kwenye haki za binadamu.

Fuatilia utagundua madudu mengi sana kwenye taasisi hii ikiwa ni kuajiri watu wasio na sifa kama TBS, ni aibu kubwa sana kwa taasisi kubwa kama hizi kufanya upendeleo kuajiri kwa kujuana na walio na sifa kukosa nafasi kitu ambcho ni knyume kabisa na taratibu za nchi yetu.

Asante na natumaini utafuatilia kwa undani swala hili.
 
Kigoda hajafanya jambo lolote la kizalendo pale TBS; kitu alichofanya ni kuteua bodi ambayo itafuata matakwa yake ya kuzipa tenda kampuni za kukagua magari ambazo hazistahili kufanya kazi hizo ili mradi akikidhi maslahi yake!!
 
Back
Top Bottom