Mheshimiwa Waziri Peleka Jeshi Shinyanga. Wananchi wako Wanauawa kila siku

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
6,651
Reaction score
14,337
Siku ya saba sasa mji wa shinyanga umekuwa mtupu baada ya lile tishio la Simba mla watu na vitu kuvamia mkoa huo. Inasemekana wananchi walisha tahadharishwa ujio wa Simba huyo na wengine waliamua kukimbia kuacha makazi yao.

Simba huyo wa miujiza amekuwa akila kila kitu anachokuta na hii ni kutokana na ushuhuda wa wananchi mbalimbal wakiwepo waliosema kuwa alikula mbao, na huko mwadui shinyanga alikula madini baada ya wachimbaj kukimbia.

Hali hiyo imeendelea leo baada ya Simba huyo kuvamia katikati ya Mji wa shinyanga na kuvunja maduka yote yaliyokuwa stand na hatimaye kula bidhaa mbalimbali yakiwepo mabasi machache yaliyokuwa yameachwa stand.

Wananchi wengi ambao walikimbilia mikoa ya jiran ya Tabora na Mwanza ili kuokoa maisha yao. Kwa hali ya sasa mji wa shinyanga umeachwa ukiwa kama vile wanachi wake walipigwa na bomb la nyuklia. Mpka sasa haijafahamika hasara iliyosababishwa na mnyama huyu. TANAPA wao wamesema hilo suala kwa sasa wameamua kuliacha chini ya Jeshi kutokana na kukosa Vifaa mujarab vya kumdhibiti Simba huyo.

Haijafahamika Mnyama huyo mwenye njaa akitoka Shinyanga atalekea wapi. Lakin kuna Baadhi ya Mikoa wameanza kuhama majumbani kwao ili kuepuka madhara yatokanayo na Simba huyo.

Tutaendelea kuwaletea Taarifa zaidi kuhusiana na Taarifa hizi za Huzuni kwa wananchi wengi ambao wamekuwa wakiomboleza kwa namna yake. Kwa kuvaa nguo nyeupe kwa imani kuwa kuna Rangi ambazo Simba huyu hapatani nazo kabisa.
 
Simba ni Taifa kubwa....Na bado Yanga Wazee wa Churani.
 
Mnyama katafuna hadi mbao [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Huyo simba atakuwa anaisoma namba vibaya sana, anakula kila kitu kwa njaa ya mwaka tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…