Nkuruma wa Karne ya 21
Member
- Jul 22, 2021
- 7
- 5
MHIMILI MMOJA KATI YA MITATU UKIWA DHAIFU MZIGO NI KWA WANYONGE.
Na Nkurumah wa Karne ya 21.
Mkichagua hovyo hovyo mtapata viongozi wa hovyo hovyo, watawaongoza hovyo hovyo, mtaishi hovyo hovyo na mtalia hovyohovyo; Bali mkichagua vizuri, mtapata viongozi wazuri, watawaongoza vizuri, mtaishi vizuri na mtajisikia vizuri.
Hakuna Jambo muhimu kwa maisha ya jamii kama uchaguzi wa viongozi na kujua namna ya wananchi kumiliki madaraka waliyonayo ili kiweza kuwadhibiti watawala wao wasitende matakwa yao Bali watende yale jamii iliyawaajiri inaulyoyataka.
Mwl. Nyerere aliamini kuwa jamii ya kusifusifu watawala, kuwaogopa na kukaa kimya huwaandaa viongozi wake kuwa madikteta.
"Msiwe watu wakuwaogopa ogopa viongozi wenu mliowachagua mkifanya hivyo mtaongozwa na madikteta, jamii lazima iwadhibiti viongozi wafuate matakwa ya watu" alinukuliwa Mwl. Nyerere katikka baadhi ya hutuba zake akilaani tabia ya kusifusifu Kila Jambo la viongozi.
Hapa kwetu bado hatujatumbukia huko, bado lakini masaka kadhaa yanayoendelea yanaonesha uwakilishi usio imara wa wananchi kutoka kwa waliowachagua.
Mwaka Jana, uchaguzi wa 2020 ulilipatia taifa viongozi karibia wote, kutoka katika chama kimoja Cha siass, CCM; Chama kikongwe, imara chenye misingi na rasilimali watu ya kutosha lakini hadi sasa miezi takribani Tisa katika majukumu yake uwakilishi wa BUNGE la Chama kimoja umerudisha maumivu kwa wananchi na viongozi wakuu.
Kwamba wabunge wamefanana kauli, hakuna Tena michuano ya hoja katika upitishaji masuala yanayohitaji maamzi bora kwa maslahi ya wengi, hakuna Tena mijadala mipana bungeni wala wabunge wanaoibuka kupambana dhidi ya Kila linaloibuka hata kama linaumiza wananchi, Leo ni wananchi wenyewe ndio wanaojitetea baada ya waliowapa mamlaka na kuwachangia pesa kwa Kodi zao kushindwa kuwatetea katika maamzi.
Kumekuwa na masakata ya Moto kuteketeza maeneo kadhaa Mara kwa Mara zikiwemo shule na Soko kuu la Kisutu Dar es Salaam lakini hakuna sauti ya mbunge iliyosikika ikitoa neno hata la kushauri ama kuhoji serikali katika namna za uchukuaji hatua, miezi kadhaa iliyopita lilitokea tatizo la umeme lilililoleta kero na usumbufu mkubwa kwa watanzania lakini hakuna sauti za wabunge zilizoliva hili ipasavyo, Ripoti ya C.A.G iliibua madudu mengi ambayo yangehitaji ufuatiliaji lakini kilichofuata ni wananchi wenyewe ndio walijaribu kuhojihoji huku bungeni akipigwa vijembe yeye na hata kuonywa akae kimya.
Kama hayo hayatoshi, Tozo Kali Sana kupitia miamala ya simu zimekuja kwa mwananchi japo zilipigiwa kelele tangu kupendekezwa kwake hata hivyo japo zimeubua kero kubwa baada ya kupitishwa na BUNGE, hakuna mbunge anayekemea wala kushauri tofauti, wote wamekaa kimyaaaaaa.
Ni wananchi wenyewe kupitia mitandao ya kijamii na vijiwe wanapaza sauti zao kulia juu ya ugumu wa maisha ulioanza tangu kuanza kwa Tozo hizi ambazo zinadaiwa kufanya wengi kuikwepa miamala ya simu kwa sasa na kutafuta njia mbadala za kutumiana pesa ikiwemo kusafirisha kwa bahasha kupitia magari ya abiria. Inasikitisha Sana.
Kufeli kwa muhimili wa serikali ni mzigo kwa wananchi na watawala wakuu.
Leo hii Waziri wa fedha Mwigulu NCHEMBA anaumiza kichwa ikiwa ni ashikilie msimamo wa Tozo ama atengue aoneshe Tozo hizi huku RAIS wetu mpendwa, aliyevaa falsafa ya amani, matumaini, demokrasia, haki na umajumui wa Utandawazi wa dunia ya sasa wakimtia doa kuonesha serikali yake inaumiza 'wanyonge'.
Maswali yanayoimiza vichwa vya wenye akili nj; Je Hawa wabunge wamefanana kauli juu ya masuala haya kwa maslahi ya Nani? Kwanini BUNGE la Chama kimoja limekosa michuano ya hoja katika maswala ya umma kwani wabunge huenda bungeni kutetea vyama ama wananchi? Kama hata Mambo yanayoonekana wabunge wanakuwa kimya, Je Kuna mangapi yanayoimiza taifa hili hayaibuliwi bungeni?.
Mbaya zaidi ni kwamba, haya yanaendelea huku taifa likiwa limesheheni vyombo vya habari vya umma na vya watu binafsi vikiwemo vya taasisi za dini, Vimekaa kimya ama vinanadi yale yanayolenga kufuruahisha viongozi tu; BUNGE lipo, Nchi Ina utitiri wa vyuo, wasomi na maprofesa wakutosha wamekaa kimya wanatafuta ajira wale waishi wazeeke na baadaye wafe huku shida za jamii ambazo walisoma ili kusaidia kuzikabili zikiwa palepale, mbaya kabisa wengine wanasifia sifia Kila Jambo aidha la vyama vyao ama la watawala ili kusaka zaidi fursa binafsi ikiwemo kubahatisha kutafuta teuzi. Oooh Nchi yangu Tanzania.
Mwana wa Lufunga nashauri; Wabunge wetu ilindeni kwa nguvu na wivu mkubwa Sana hadhi ya CCM, hiki ni Chama kikubwa, imara chenye katiba yenye miongozo mitamu Sana ya utu, uzalendo na ujamaa, acheni kuifanya 2024 na 2025 ije iwe kazi nzito balaa kuwatetea viongozi wetu kwa wapiga kura; Nashauri Mheshimiwa Rais kuwa mstari wa mbele kuchukua maamzi ya haraka katika masuala yanayoumiza jamii kwani kwani ni yeye ndiye anayechafuka kutokana na makosa ya wasaidizi wake, Nashauri Viongozi kuendelea kujazwa hakema za Mwenyezi Mungu ili badala ya kukerwa na malalamiko ya watu dhidi ya maamzi yao na wajue uongozi upo ili kutatua kero za watu na si watawala kutimiza watakayo wao kwa watu
Kiongozi anaweza kuwa na Jambo jema Sana lakini ikiwa jamii hailitaki ajiulize tu wema wake huo ikiwa wananchi wengi wasingempa kura angekuwa katika nafasi hiyo? Basi kwakutumia falsafa hii viongozi wetu jaribuni kutusikiliza sisi wa chini kwanj mpo ili sisi Nazi japo hatuna hata kazi na mishahara tuweze kupata nafuu ya maisha na si tulie na kuumia kisa kiongozi fulani amelipenda.
Utawala wa King Luis wa 16, Mtawala wa kifalme wa zamani huko Ulaya uliangushwa kutokana na kauli yake moja tu aliyonukuliwa akisema "Jambo ni jema na linahitajika Uingereza ikiwa Mimi ninalitaka lakini Jambo ni haramu na halitakiwi kwa Waingereza ikiwa mie silitaki" aliondoshwa mapema Sana baada ya kauli hii.
Mandela, Mwana wa Afrika aliyewahi kuwa nguli wa siasa za dunia aliamini kuwa mtu hawezi kuwa na mchango wa mageuzi katika jamii asipokubali kubadilika yeye mwenyewe kuendana na matakwa ya wakati.
"Hauwezi kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii ikiwa hauwezi kubadili mitazamo yako wewe mwenyewe" alitamka Nelson Mandela akiwataka Viongozi kuendelea kujisahihisha na kujua matakwa ya watu na wakati.
Suala la kusifusifu Kila Jambo aidha kukosoakosoa tu Kila Jambo kwa misingi ya kujipendekeza, ama kukaa kimya hata kwa yale ungeweza kuyatatua, tabia ya kukejeli Mambo leo na kuyaunga mkono kesho kwa sababu ya kutaka fursa binafsi ni usakatonge hatari uliotufikisha hapa, dhambi kubwa inayotafuna maendeleo yetu kwa sasa ni jinsi tunavyofikiri na kutenda.

Upvote
2