Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira Arusha, Alexanda Bakunguza, amefungua kesi Mahakama Kuu dhidi ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali akipinga elimu ya juu kugharamiwa na serikali kwa njia ya mikopo.
Katika kesi hiyo namba 16 ya mwaka 2021, mhitimu huyo anatetewa na mawakili watatu kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ambao ni Mpale Mpoki, Steven Mwakibolwa na Amani Jowachim.
Kesi hiyo iko chini ya majaji watatu wa Mahakama Kuu ambao ni Jaji Victoria Makani, Jaji Benihaj Masoud na Jaji Opiyo.
Mhitimu huyo anadai hoja yake ya msingi ni kwamba tozo na riba katika mikopo wanayopewa wanafunzi wa elimu ya juu inamchelewesha mwanafunzi kupata maendeleo japokuwa ameshaelimika.
Kufuatia hali hiyo, anadai elimu ya juu igharamiwe na serikali kuanzia mwanzo wa masomo hadi mwisho bila mwanafunzi kulipishwa gharama yoyote.
Msingi wa madai hayo unatokea kwenye Ibara ya 11 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaeleza kuwa serikali itafanya jitihada kuhakikisha watu wote wanapata fursa sawa na za kutosha kuwawezesha kupata elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za shule na vyuo vinginevyo vya mafunzo.
Hata hivyo, kesi hiyo imewekewa mapingamizi matatu na serikali ikisema haina mashiko hivyo ifutwe.
Kesi hiyo ilifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Julai 29, mwaka huu na jana ilitarajiwa kutolewa uamuzi juu ya mapingamizi yaliyowekwa na serikali.
Ippmedia