Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Ukichunguza kwa makini utagundua moja ya athari ya watu kuhamia mijini kutoka vijijini ni vijana wengi kuzaliwa na kukulia mijini kias kwamba wengi hawapati fursa ya kujifunza lugha zao za asili kama ilivyo kwa wale wanaozaliwa vijijini waliko wazee.
Wazazi wengi huku mijini wanaacha ule utamaduni wa kuwaongelesha kilugha watoto wao tangu utotoni na badala yake wanakuwa wakijifunza kiswahili na wengine kingereza kwa wale wanaosoma shule hizi za kisasa.
Baadhi ya watoto hawa wengine hata kiswahili hawakijui bali wanajua zaidi kingereza kutokana na muda wote kuongea kingereza shuleni, na hata wakirudi nyumbani ni ndani ya mageti huku wakiongea kingereza na wazazi wao.
Sasa hawa watoto lugha zetu za asili (makabila) ndio kabisa hawataka wayajue kwani hata salamu tu ni mtihani.
Siku hizi hata ule utamaduni wa kuwapeleka watoto vijijini kwa babu na bibi zao haupo acha ule wa kuacha watoto kulelewa na babu/bibi, utamaduni uliosaidia watoto kujifunza lugha za makabila yao kwa kuongea kilugha na babu,bibi, wajomba, mashangazi na ndugu na jamaa wengine waliko vijijini.
Ukichunguza utagundua hali hii ilianza kujitokeza kidogo kidogo kwa wale waliozaliwa miaka ya 70 na kuendelea watu walipoanza kuishi katika nyumba (kota) za serikali, watu kuhamia na kujenga mijini kutoka vijijini.
Kwahiyo, katika kipindi hiki cha miaka 50, utagundua hali hii inazidi kuongezeka na hivyo ndani ya miaka 150 mpaka 200 ijayo, idadi ya watu wasiojua lugha zao za asili inaweza kuongezeka mara tatu mpaka mara nne ya hali ilivyo sasa na kuziweka lugha zetu za asili katika hatari ya kuanza kutoweka kabisa na tukabaki na kiswahili na kingereza.
Mwisho, kama ambayo leo hii tunalaumu wazungu kwa kudhoofisha mila na desturi zetu, ndivyo hivyo hivyo tutakuja kulaumu wazungu kwa kuua lugha za makabila yetu wakati chanzo ni sisi wenyewe.
Kuna uwezekano identify ya mtu mweusi itabaki kuwa ni rangi yake ya asili na pengine akili yake ikilinganishwa na akili za wenzetu.
Tatizo hili linakwenda na linaoongezeka mithili ya tatizo la climate change linaoongezeka huku jamii ikilipuuza kwasababu tu linaongezeka kidogo kidogo lakini madhara yake teyari yapo na sasa yanaanza kuwa dhahiri .
Mimi kuongelea jambo hili sasa, kutapokelewa mithili ya watu walivyopokea tatizo la climate change katika karne ya 20 wakiona ni kitu ambacho hakipo.
Muda utaongea.