Miaka 150 mpaka 200 ijayo, lugha zetu za asili nyingi zitakuwa zimetoweka

Wapuuzi sana hao watu. Mtu hajui kuongea lugha yake ya asili,hajui kuimba wala kucheza ngoma zao za asili. Wana bahati sana tuko kwenye mfungo ningewatukanilia mbali
Nalog off
 
Lengo la hizi lugha ni kuelewana.

Na wala sio lengo kuwa na lugha nyingi

Zamani ilikuwa ule mukngiliano baina ya watu wa sehemu fulani na fulani haukuwepo,hii ikapelekea kila kikundi kuwa na lugha yake ambayo itaelewana na watu wa hapo hapo kwao.

Watu walipotembea wakaingiliana ndipo zikazaliwa lugha ambazo wangeweza kuelewana kinyume na lugha zao za asili.

Sasa kama sasa hivi hizo lugha zina maana gani wakati tuna lugha ya kiswahili ambayo inakidhi vigezo vyote ?

Ikiwemo kuelewana baina ya watanzania kuliko lugha zingine na kurahisisha mawasiliano.

Leo mtu ukienda kariakoo ukaongea kimakonde kutaka msaada watakaokusaidia ni wamakonde tu)lakini ukiongea kiswahili watanzania wote wa pale watakuelewa.

Hivyo hata hizo lugha za asili zikipotea ni ishara ya maendeleo
 
I agree. Na tena inawezekana tukawa na lugha moja dunia nzima huko mbeleni...
Umefikiri vizuri mno!

Ninakubaliana na wewe kwamba huko mbeleni,kwa kusaidiwa na maendeleo na mapinduzi makubwa katika teknolojia ya habari,to be specific, kiingereza itakuwa lugha ya Dunia.

Najua kuna watu hawapendi kiingereza,lakini hiyo haibadilishi kitu! Lugha hii adhimu inazidi kukua na kusambaa kote duniani. Leo wachina wanalazimika kujibatiza majina ya kizungu ili waweze kuuza bidhaa zao duniani.
 
Na pia lugha ya Alama itachukua hatamu sana yaani emojies
 
Bado sana. Nenda umasaini kaongee nao kiswahili na kizungu.
Hata hivyo mabadiliko ni lazima. Dunia inaenda kuwa kijiji, na watakaokuwepo watazungumza lugha chache sana.
 
Lugha ya kisukuma kufutika labda miaka elfu 4 ijayo.
Ukichunguza vizuri historia ya wasukuma,kabila hilo halijafikisha hata miaka 800!

Kwa kabila ambalo umri wake ni huo,unadhani kitu gani kitazuia lugha yao kupotea?

Utabiri wangu,miaka 100 mbele hakuna binadamu atakuwa anazungumza kisukuma!. Ukitaka kusikia kisukuma,wakati huo,utalazimika kwenda Bujora Sukuma Museum!
 
M
Binafsi sioni faida ya hizo lugha

Japo mwenyewe nilitumia nguvu kubwa sana kujifunza kilugha maana wazee wangu hawakuwa wakiongea na sisi japo wote wanatoka kabila moja


😂
 
Nilifungua uzi huu hapa chini lakini nikaishia kushambuliwa. Wazungu wameona umuhimu na wanatunza lugha za mataifa na makabila mbalimbali.

Unaweza ku promote makabila bila ukabila
 
Hujielewi kabisa
 
Mimi nadhani hakuna haja ya kupigania vitu vingine...

Kama kitaishi kiache kiishi. Ikishibdikana poa. Kwani vingapi vilikuweko kitambo leo havipo..?
 
Watoto wa Lissu hawajui kinyiramba kama ambavyo watoto wa Mbowe wasivyojua kichaga. Uko sahihi kamanda
 
Mimi nadhani hakuna haja ya kupigania vitu vingine...

Kama kitaishi kiache kiishi. Ikishibdikana poa. Kwani vingapi vilikuweko kitambo leo havipo..?
Mimi nimeamua kulisema hili mapema ili lika kutokea, tusianze kulaumu wasiohusika na pia lisitushangaze.

Jambo kama hili sio rahisi kulifikiria wala kuli-note na huu ndio udhaifu wa sisi binadamu na hata unapoliongea, wengi hawakuelewi kabisa.Hivyo the best way ni kuliweka katika maandishi(vitabu) kwa rejea ya vizazi vijavyo.
 
Binafsi sioni faida ya hizo lugha

Japo mwenyewe nilitumia nguvu kubwa sana kujifunza kilugha maana wazee wangu hawakuwa wakiongea na sisi japo wote wanatoka kabila moja
Lugha zote zife tu na makabila yote yapote tu
Itaondoa mambo ya ukabila

Ova
 

Hizo lugha zitoweke tu tubaki na lugha moja ya Taifa. Nafikiri itasaidia kupunguza majivuno, dharau, chuki nk. Hivi hapa JF kama kila mtu angekuwa anaweka bandiko kwa lugha yake ya asili ingekuwaje?
 
Nakubaliana nawe kuhusu Utumwa wa fikra kiasi cha kutukuza ugeni. Lakini kwa Tz si suala la ushamba, bali ni utaifa. Tumetumia nguvu na muda mkubwa kutengeneza taifa moja. Sisi ni taifa. Hao wanaijeria hawana taifa, ni mkusanyiko wa nchi nyingi ndani ya mpaka mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…